Pangani FM

UZIKWASA yawakutanisha viongozi wa vyombo vya Habari Tanzania

13 March 2023, 2:18 pm

Baadhi ya washiriki wa mafunzo yanayoendelea katika moja ya Ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma. Picha na Erick Mallya.

Kwa miaka mingi Shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya ‘mguso’ ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutafakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi na Jamii kwa ujumla.

Mwezeshaji kutoka Shirika la UZIKWASA Bi, Maimuna Msangi akiendesha sehemu ya mijadala katika mafunzo hayo yanayoendelea Jijini Dodoma.

Na Erick Mallya

Shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani Mkoani Tanga kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeanza rasmi mafunzo maalumu ya siku 4 yanayowakutanisha viongozi waandamizi wa vyombo vya Habari vya Tanzania bara na visiwani yenye lengo la ‘kuwezeshana kwa pamoja kama viongozi wa vyombo vya Habari juu ya kutafakari na kuzingatia masuala ya jinsia kwa kutumia mbinu wezeshi (Mguso)

Mkurugenzi wa kituo cha Redio Irangi FM iliyopo Mkoani Dodoma Bi Saumu Sakala akizungumza katika mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yanaendelea katika moja ya kumbi za Royal Village zilizopo jijini Dodoma kuanzia Machi 13-16, 2023.

Mwezeshaji Kutoka Shirika la UZIKWASA Bi. Salvatha Kalanga akiendesha sehemu ya mijadala ya mafunzo hayo.

Kwa miaka mingi shirika la UZIKWASA limekuwa likitoa mafunzo ya mguso ambayo yamekuwa yakiwawezesha watu binafsi kutakari nafasi zao katika kuchochea mabadiliko chanya pamoja na mabadiliko ya kitaasisi.

Bi Zania Kweka Kiogozi kutoka Dodoma FM iliyopo jijini humo akichangia mjadala.

Wanufaika wa mafunzo hayo wamekuwa vongozi wa dini, viongozi wa taasisi, waandishi wa habari, vongozi wa kisiasa na wale wanaosimamia masuala ya Jinsia na Mazingira.

Faida za mafunzo hayo zimetambulika katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.

Mkuu wa Kituo cha Redio Fadhila iliyopo wilayani Masasi Mkoani Mtwara Bw. Edwin Mpokasye akizungumza katika moja ya mijadala iliyoibuka ndani ya mafunzo hayo.Picha na Erick Mallya

Mafunzo hayo yanatarajiwa pia kuwajengea viongozi hao  uwezo wa kujtathmini, kusikiliza,kuwajibika,kuwawezesha wengine kuwa kufikia uwezo wao na kufanya kazi katika mazingira ya timu, kuboresha mahusiano na mawasiliano na kutengeneza maswali ya kimkakati ili kuhakikisha masuala ya Jinsia yanazinagtiwa ndani na nje ya vyombo vya Habari.

Mshauri wa masuala ya vyombo vya Habari Bi. Lillian Urio  kutoka Dar es Salaam akizungumza wakati wa mjadala wa masuala ya Jinsia ndani ya vyombo vya Habari.

Vongozi hawa wa vyombo vya Habari wanatarajiwa kuwa sehemu ya uwezeshaji wa waandishi wa habari katika umahiri wa kufanya kazi zao kwa kuzingatia masuala ya jinsia ndani nan je ya vyombo vya Habari.

Bi Gladys Mapeka Meneja wa Redio Kilosa FM ya Mkoani Morogoro akizungumza katika moja ya mijadala inayoendelea katika mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yatafuatiwa na mafunzo kwa waandishi wa Habari wa vituo 15 vya Tanzania bara na visiwani baadae juma hili.

Bw, Ally Khamis Mtwana wa Adhana FM ya Mjini Magharib Unguja, Zanzibar akizungumza wakati wa mafunzo hayo.