Pangani FM

UZIKWASA yapongezwa kwa hili 2023

13 February 2023, 4:32 pm

Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Kwakibuyu wilayani Pangani akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa uoto wa asili. Picha na Erick Mallya

Na Erick Mallya

Wadau mbalimbali wa mazingira wilayani Pangani Mkoani Tanga wamelishukuru shirika la UZIKWASA kwa kuanza kutoa mafunzo ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na utunzaji wa mazingira wilayani humo.

Kuanzia Februari 7 mpaka 10  shirika hilo kwa kushirkiana na halmashauri ya wilaya ya Pangani Mkoani Tanga limetoa mafunzo kwa kamati ya mazingira ya kijiji cha Kwakibuyu kilchopo wilayani humo yaliyokuwa  na lengo la kuijengea uwezo kamati hiyo katika kuhusisha masuala ya jinsia katika mipango kazi yao.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakijadili wakati wa mafunzo

Wakizungumza na Pangani FM wajumbe wa kamati ya mazingira ya kijiji cha kwakibuyu  wameeleza hisia zao kufuatia shirika la UZIKWASA kuanza utekelezaji wa afua za mabadiliko ya tabia nchi na jinsia.

“Naitwa Sheikh mbwana Riko Abdalha, ni sheikh wa kata ya Kipumbwi ni bora sana kwa UZIKWASA kufanyia kazi masuala haya sababu elimu hii tunaweza kuwarithisha hata watoto wetu”

“Nitoe shukrani zangu za dhati nashukuru sana uzikwasa kwa kutupa elimu hii mmi na kamati yangu tutayafanyia kazi mafunzo haya”

Bila ya UZIKWASA elimu hii isingekuwa nayo, hali ilishakuwa n mbaya lakini kwa kutuletea elmu hii nalipongeza sana shirika la UZIKWASA”

Wamesema wadau hao.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Hussein Aweso amesema kuwa maa baada ya kupatiwa mafunzo hayo yeye na kamati yake watakuwa katika nafasi nzuri ya kuchukua hatua dhidi ya Uharibifu wa mazingira na Mabadliko ya Tabia nchi katika kijiji chao.

“Mengi ilikuwa hatuyaelewi ila sasa tunayaelewa sasa mimi na kamati yangu tutahmiza utaratibu ambao utakuwa tofauti na zamani kwa hiyo utasadiana kuhamasisha wananchi kwa hii semina tuliyopata kutoka UZIKWASA”

Amesema Mwenyekiti wa Kijiji cha Kwakibuyu

Pangani FM imezungumza pia na Mkuu wa Idara ya Mazingira Halmashauri ya wilaya ya Pangani bwana Daudi Mlahagwa ambaye ameeleza kuwa Kutokana na ukubwa wa shirika la UZIKWASA na uzoefu wake katika kutoa elimu itakuwa msaada mkubwa kwa Idara yake.

Suala la UZIKWASA kuwa na afua za mazingira ilikuwa ni kilio changu cha muda mrefu sana na nashukuru kwamba yale mawazo yetu ya mwanzo yameanza kufanyiwa kazi UZIKWASA ni shirika kubwa linahusisha wadau wengi na limekuwa na uzoefu mkubwa kwenye kutoa elimu kuingia katika afua za masuala ya mazingira imekuwa ni kitu kizuri kwa jamii yetu ya Pangani, sasa hivi kwa vile wanahusianisha ukatili na masuala ya jinsia kwa hiyo yale masuala yanayoimbwa kimataifa yanatkelezwa kwa ukaribu sana na shirika letu, nashukuru kwa sababu sasa imeigia kuwa mdau wa muhimu wa mazingira

Amesema Daudi Mlahagwa Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya Pangani.

Hayo yamejiri katika mafunzo ya siku nne ya kuijengea uwezo kamati ya mazingira ya kijiji cha Kwakibuyu wilayani Pangani Mkoani Tanga katika kuhusisha masuala ya kjisnai kwenye mipango kazi yao.

Mafunzo hayo yaliyoanza Februari 7 yamekamilika siku ya Ijumaa Februari 9 ikiwa ni sehemu ya Afua ya shirika la UZIKWASA ya Mabadiliko ya tabia nchi na Jinsia.