Pangani FM

Yaliyoibuka kwenye ziara ya kushtukiza ya DC kwenye soko la Pangani

8 February 2023, 12:08 pm

Mkuu wa Wlaya ya Pangani akiwa katika moja ya maeneo ya soko hilo. Picha na Ofisi ya DC Pangani

Soko la Pangani liko kwenye maboresho makubwa yaliyoplekea kituo cha mabasi ya Pangani-Tanga na Pangani-Muheza kilichokuwa ndani ya Soko hilo kuhamishwa ili kupisha maboresho hayo.

Kwa miaka mingi soko hilo limekuwa taswira ya mji wa Pangani na kituo maarufu kwa wageni wanaofika kwenye mji huo kwa matembezi na manunuzi ya bidhaa za Pangani.

Saa Zumo & Erick Mallya

Serikali wilayani Pangani Mkoani Tanga imeahidi kuboresha soko la mbogamboga wilayani humo ili liweze kuendana na mahtaji ya wajasiriamali pamoja na uliwekea mazingira rafiki kwa wateja wanatumia soko hilo katika manunuzi ya mahitaji ya kila siku.

Baadhi ya vibanda katika Soko hilo.

Hayo yamejiri Februari 7 katika ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Mkuu wa wilaya hiyo Bi.Zainab Abdallah Issa ili kusikiliza kero na changamoto za wajasiriamali wa soko hilo ambao sehemu kubwa ni wanawake.

“Changamoto kubwa ni kuhusu mazingira ya hili soko, kipindi cha jua mnapata changamoto na hata kipindi cha mvua mnapata changamoto, sasa DAS aelekezo yangu leo nikitoka hapa Injinia arudi na kesho Asuuhi nataka majibu ya mustakabali wa hili soko kama inawezekana nijue na kama haiwezekani nitajua mwenyewe nitafanya nini”

Amesema DC Pangani Bi.Zainab Abdallah Issa