

2 February 2023, 9:01 pm
Na Saa Zumo kushirikiana na Erick Mallya
Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Issaya Mbenje kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa mahakama ya kisasa.
Agizo hilo amelitoa katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria wilayani Pangani yaliyofanyika katika vwanja vya mahakama ya wilaya pamoja na kuahidi kutoa kipaumbele kwa masuala ya Mahakama ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi Pangani.
“Bila kuishika hii tasisi na mhimili huu muhimu hatuwezi kwenda kwa sababu kama wanadamu lazima kutatokea ukiukwaji wa sheria na migongano sasa hiki chombo ndio kinasaidia kufanya utatuzi na usuluhishi”
Amesema Bi.Zainab Abdallah Issa