Pangani FM

DAS Pangani atangaza hatua dhidi ya wazazi wasiochangia chakula Shuleni

31 January 2023, 11:56 am

Katibu tawala (DAS) wa wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange. Picha na Erick Mallya

Jumla ya wanafunzi 280 walifanya mitihani ya Darasa la Saba mwaka 2022 katika shule ya msingi Kipumbwi. Waliochaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari ni 219 na ambao hawakufanikiwa kupata alama za kutosha kuendelea na elimu ya Sekondari ni 61.

Na Saa Zumo kushrikiana na Erick Mallya

Kufuatia Shule ya msingi ya Kipumbwi wilayani Pangani Mkoani Tanga kufanya vibaya katika mitihani ya Darasa la Saba mwaka 2022, Katibu Tawala wilayani humo Mwalimu Hassani Nyange amefanya kikao na wazazi na walezi wa wanafunzi mbalimbali wa shule hiyo ili kutathmini changamoto zilizopelea wanafunzi hao kutofanya vizuri na kuweka mikakati ya kuboresha ufaulu kwa mwaka 2023.

katika kikao hicho moja ya changamoto iliyotajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa matokeo mabaya shuleni hapo ni tabia ya baadhi ya wazazi kukataa kuchangia chakula shuleni.

Suala la chakula nitalisimamia mwenyewe,watoto wote watakula chakula sababu itakuwa ni maazimio ya kijiji, haiwezi kuzidi elfu 35 kwa mwaka mpaka darasa la Saba waondoke, watakaokataa wote watapelekwa mahakama ya Kipumbwi, wale ambao wana uwezo na wamefanya makusudi watachukuliwa hatua tofauti

Amesema Katibu Tawala Wilaya ya Pangani Mwalimu Hassan Nyange.

Mwanahabari wetu Saa Zumo amehudhuria kikao hicho, sikiliza hapa taarifa aliyotuandalia.

Taarifa zaidi juu ya umuhimu wa kuwepo kwa programu za chakula shuleni na mchango wake katika kuchochea ufaulu