Pangani FM

Marufuku Bidhaa za Misitu kubebwa kwenye Pikipiki Pangani.

28 June 2022, 6:30 pm

Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) wilayani Pangani mkoani Tanga imepiga marufuku ubebaji wa mazao ya misitu ikiwemo mkaa kwa kutumia pikipiki ikiwa ni sehemu ya kupunguza mianya ya utoroshaji wa mazao hayo kwa njia za magendo.

Afisa mhifadhi wa misitu wilaya ya pangani Bw. John Kimario  amesema licha ya kufunguliwa kwa maombi ya uvunaji wa misitu ni vyema waombaji wakatambua kuwa watalazimika kutumia magari badala ya pikipiki katika kubeba mazao ya misitu.

‘Mwaka huu hatutazamii pikipiki kubeba mazao ya misitu kwa sababu usimamizi wa pikipiki unahitaji tahadhari zaidi kwa sababu pikipiki inaweza kupita njia zile ambazo ni tofauti na ile iliyoandikwa kwenye kibali, mfumo wetu wa usafirishaji na kutoa vibali vya mazao ya misitu pikipiki hazipo badala yake inatakiwa tutumie magari ndio maana nikasema kwamba mwaka huu pikipiki hatutozitumia labda kamamtu ana gunia mbili za mkaa ametoa shambani kwake na sio kwa ajili ya Biashara, lengo kubwa ni kuepusha kutorosha mazao ya misitu ukizingatia wilaya ya Pangani bado tunazo Bandari bubu amabazo zinatupa kazi kukabiliana nazo mpaka sasa hivi’Amesema Bw. Kimario.

 

Aidha atika kuboresha uvunaji endelevu wa misitu wakala wa huduma ya misitu wilaya ya Pangani umetangaza utaratibu wa kuomba kibali cha uvunaji mara moja kwa mwaka na kuwataka wananchi kuhakisha wavunaji wanachangia masuala ya maendeleo katika vijiji vyao.

Wakala wa huduma za misitu Tfs wilayani pangani tayari wametangaza maombi ya vibali vya uvunaji kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ambapo maombi hayo yatadumu hadi Julai mosi mwaka huu.

 

 

 

 

Picha kwa hisani ya Congo in Conversation