Pangani FM

Miche 300 ya Mivinje yapandwa Pangani kuadhimisha siku ya mazingira.

6 June 2022, 5:10 pm

 

Viongozi mbalimbali wa wilaya ya Pangani wamejitokeza katika zoezi maalum la upandaji miti kama sehemu ya kuadhimisha  siku ya mazingira mwaka 2022.

Zoezi hilo lililofanyika katika fukwe za eneo la Pangadeco limewezesha upandaji wa miche  300 ya miti aina ya Mivinje.

Zoezi hilo limefanywa na viongozi hao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira ikiwemo kutoka taasisi ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira iliyojikita katika upandaji na utunzaji wa miti ya foundation for trees Tanzania, chuo cha usimamizi na uongozi wa Wanyama pori MWEKA pamoja na BMU.