Pangani FM

IRISH AID yafurahishwa na kazi za UZIKWASA Pangani.

6 June 2022, 7:12 pm

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ireland, Bw. Joe Hackett, amefanya  ziara wilayani Pangani Mkoani Tanga  akiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Ireland (Irish Aid), Bw. Michael Gaffey.

Katibu huyo amefika katika kijiji cha Kimang’a kilichopo wilayani humo na kukutana na baadhi ya makundi mbalimbali yanayofanya kazi katika afua mbalimbali za kupambana na ukatii dhidi ya wanawake na watoto kupitia  shirika la UZIKWASA.

Ziara hiyo imefanyika siku ya Jumamosi Juni 4,2022.

Picha: Katibu Joe Hacket, Balozi wa Ireland Nchini Bi. Mary O’Neil pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bw. Ghaibu Buller Lingo akiwa na wafanyakazi wa UZIKWASA na wadau wake.

 

 

Makundi hayo ni Kamati za MTAKUWWA, wawezeshaji ngazi ya jamii, waigizaji pamoja Bodaboda ambao wamepatiwa mafunzo na shirika la UZIKWASA.

 

Akiambatana na viongozi wa wilaya ya Pangani wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Bw. Ghaibu Buller Lingo katibu huyo alipata nafasi ya kuzungumza na makundi hayo ambapo alipata nafasi ya kupata uzoefu wa namna wanavyofanya kazi na kunufaika na shirika la UZIKWASA.

Picha: Mkuu wa wilaya ya Pangani Bw. Ghaibu Buller Lingo pamoja na Katibu Joe Hacket 

Aidha Bwana Joe Hacket ameelezea kufurahishwa kwake na namna shirika laUZIKWASA lilivyoweza kuwakutanisha wadau mbalimbali wa wilaya ya Pangani katika kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii na hatimaye kuweesha kizazi salama dhidi ya vitendo vya ukatili na kuahidi kuwa IRISH AID itaendelea kufanya kazi na shirika la UZIKWASA ili kuendeleza kazi nzuri inayofanya katika jamii ya Pangani.

Pia Bw. Hacket alipata fursa ya kuwasalimia wakazi wote wa Pangani kupitia Pangani FM.

Ziara hiyo imekuwa ni fursa muhimu kwa Katibu Mkuu kushiriki na kushuhudia shughuli za Ubalozi, ushirikiano, na miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Serikali ya Ireland nchini Tanzania ambayo imekuja katika  kipindi ambacho Ubalozi wa Ireland unajiandaa kuzindua Mkakati wake wa mwaka 2022–2026, ambao unaendeleza mahusiano ya Ireland na Tanzania yaliodumu kwa miaka 43. Mkakati huo unategemewa kuchangia kiasi cha Euro 110 milioni kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kupitia Ubalozi wake jijini Dar es Salaam.