Pangani FM

Pangani kutumia Milioni 35 kuwalinda Wanafuzi dhidi ya Uviko-19.

16 November 2021, 1:11 pm

Halamshauri ya wilaya ya Pangani inajipanga kutumia kiasi cha fedha Shilingi Milioni 35 kujenga miundombinu ya kuwezesha wanafunzi kunawa mikono katika shuleni kama hatua ya ujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Katika mazungumzo aliyofanya na Pangani FM Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Bw.  Isaya Mbenje amesema kuwa miundombinu hiyo itajengwa katika Shule za msingi za Kipumbwi Pwani, Madanga na Sekondari Kipumbwi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwana Isaya Mbenje.

“tumepata fedha ya kujenga mundombinu ya kunawa mikono kuna shule ya Msingi Kipumbwi Pwani, Shule ya Msingi Madanga pamoja na Shule ya Sekondari Kipumbwi wamepata fedha za kuvuna maji ya mvua na kutengeenza miundombinu ya kunawa mikono kuna Shule nyingine zilizpitia Programu nyingine  kwa hiyo watajenga vyoo, lakini pia tumeoata fedha za uhamasishaji ambazo kamati za uhamasihaji kuanzia ngazi ya Wilaya zitahakikisha tunapambana na UVIKO-19 na tumeshaokea chanjo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuchanja kujilinda na UVIKO-19”

Amesema Bwana Mbenje.