Pangani FM

Mmoja ashukiwa kufariki kwa Corona Pangani

20 July 2021, 8:06 pm

Hospitali ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga imethibitisha kifo cha mtu mmoja kutokana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na Virusi vya Corona ambavyo vimeripotiwa kuwa katika wimbi la tatu hivi sasa (DELTA).

Hayo yamesemwa na Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani Dkt HASSAN MSAFIRI katika katika mahojiano maalum aliyofanya na Pangani FM hii leo.

ninachoweza kusema ni kwamba washukiwa wapo na kifo kimoja,wilayani Pangani na washukiwa wapo ndio maana tumeamua kuja kuzungumza na wananchi hiki si kitu cha kuhamaki bali ni kitu cha kukipokea na kuweka katika akili zetu hatua za kuchukua ili kujilinda

Amesema Dokta Hassan Msafiri

Msikilize hapa Dokta Hassan (Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya ya Pangani.

Dokta Hassan Msafiri Mganga Mfawidhi Hospitali ya Wilaya Pangani

Kwa mujibu wa Dokta Hassan wapo wagonjwa watatu mpaka sasa wanaohisiwa kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona katika Hospitali ya Wilaya na sasa hivi dalili zimebadilika ambapo awali wagonjwa walikuwa wanakuja na dalili kama kubanwa na pumzi ila kwa sasa zipo dalili tofauti.

sasa kubanwa na pumzi imekuwa dalili au hatua ya mwisho, sasa hivi wagonjwa wanakuja Hospitali wakiwa wagonjwa wengi ghafla wanapata homa na kukohoa au wanaweza kuwa na dalili tatu kati ya zifuatazo homa, kukohoa, mwili kuchoka, kichwa kuuma, misuli kuuma au kupata sore throat au koo kuwasha, mafua kutoka kwa wingi au saa nyingine kubanwa na pumzi, kutapika, kusikia kichefuchefu, kuharisha na pia kupoteza hali ya akili, hizi ni dalili zinazweza kuanza mwanzo mwanzo

Amesema Dokta Hassan

Kwa mujibu wa Dokta Hassan ugonjwa huo kwa sasa upo katika ngazi ya jamii tofauti na awali ambapo ulikuwa kwa wasafiri au watu waliokuwepo kwenye maeneo yenye maambukizi na pia amewataka wananchi kutosubiri kubanwa na pumzi bali kuchukua hatua mapema pale wanaposikia dalili kama homa kali, mafua, kuharisha sana, kupoteza hamu ya kula au koo kuwasha wafike hospitali kwani hizo zimewekwa kama dalili za washukiwa wa Covid-19.