Pangani FM

UZIKWASA yawakutanisha wadau kujadili Mabadiliko ya Tabia Nchi Pangani.

14 July 2021, 7:40 pm

Wadau wa Mazingira Wilayani Pangani Mkoani Tanga wamejadili suala ya mabadiliko ya tabianchi na uhusiano wake wa kijinsia, ambapo wanawake wanaelezwa kuguswa moja kwa moja na mabadiliko hayo, na hivyo kuna umuhimu wa kuwashirikisha katika ngazi ya majadiliano.

Akizungumza na Pangani FM Mratibu wa TASAF Wilayan Pangani Bi. Asnat Mtei ambae ni mshiriki wa mafunzo ya mzingira yanayofanyika katika ukumbi wa SEA SIDE Mjini Pangani, amesema nishati ya kupikia na maji vinauhusiano mkubwa na maisha ya mwanamke, hivyo ni vyema jamii kuwashirikisha wanawake katika masuala ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

watu wanakata miti wanaharibu misitu na vyanzo vya maji kwa vile wanawake wamepewa majukumu mengi wanaenda mbali kufuata kuni na maji na hii inawanyima nafasi ya kufanya mambo mengine,jamii kwa ujumla haijamchukulia mwanamke kama kiungo muhimu katika utunzaji wa mazingira, wanawake wanapaswa kujitokeza zaidi hata katika Mikutano ya kijiji wajitokeze watoe maoni yao hususan katika amsuala ya mazingira ili kuleta maboresho kwenye jamii.

Amesema Bi Asnath Mtei

Kwa upande wake, Afisa Kilimo Kata ya Mikinguni Bi. FLORIDA KAMBONA amesema kuwa ni wakati sasa kwa wadau na viongozi kuwakumbusha wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira na matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo.

Kwa mujibu wa Jarida la umoja wa Mataifa la Wanawake la mwaka 2020 juu ya mabadiliko ya tabia nchi,majanga na ukatili wa kijinsia imeonekana kuwa ukatili uongezeka zaidi pale majanga kama mafuriko,ukame na mengine na hata baada ya kutokea kwa majanga hayo.

Hii ni kutokana na matukio kama ubakaji,wanawake kubeba sehemu kubwa ya majukumu ya familia na watoto kulelewa na mzazi mmoja (mama) kutokana na Baba kuhama kwenda kwenye eno lenye upatikanaji wa chakula, malisho ya wanyama na maji ya kutosha.

Visa vya wanawake kubakwa au kudhalilishwa  wakiwa njiani kufuata maji ambayo vyanzo vyake vimeathiriwa na mabadiliko ya Tabia nchi navyo vimekithiri.

Hayo yamejiri katika siku ya 2 ya Mafunzo ya Mazingira kwa wadau Wilayani Pangani yanayoratibiwa na shirika la Uzikwasa kwa kushirikiana na Shirika la SMECAO lililopo wilayani Same Kilimanjaro.