Pangani FM

MTAKUWWA Ubangaa waandaa eneo la Ujenzi wa Zahanati

10 May 2021, 7:04 pm

Kamati ya MTAKUWWA ya Kijiji cha Ubangaa wilayani Pangani Mkoani Tanga kwa kushirikina na Serikali ya kijiji hicho inandaa eneo kwa ajili ya ujenzi wa zahanati.

Baadhi ya Wanakamati hao wakifyeka eneo la ujenzi wa Zahanati

Wakizungumza na Pangani FM wakati wa zoezi la kufyeka eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi huo wamewataka wananachi wengine kujitokeza katika shughuli za kijamii za kujitolea.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ubangaa Bwana Robert Gaspal Komba amesema baada ya makubaliano na wananchi tayari wameshirikiana na wataalamu na kupatiwa tathimini itakayo waongoza.

“Kamati ya MTAKUWWA iliibua ikaleta kwangu,baada ya hapo tukawaona wahandisi wakatupatia gharama nzima za ujenzi (BOQ) ambapo itagharimu kiasi cha shilingi million 50,hivyo mbali na nguvu za wananchi pia tutashirikisha wawekezaji waliopo Kijijini kwetu kusaidiana katika hilo”

amesema Mwenyekiti huyo.

Mtendaji wa Kijiji hicho Bi Fatuma Mnyamisi Mhaka amesema baada ya maridhiano kupitia mkutano wa Kijiji wamekubalina wananchi kuchangia kiasi cha fedha na nguvu kazi katika hatua za awali za ujenzi wa zahanati hiyo.