Pangani FM

Sauti za Wanawake tu Kusikika Pangani FM.

8 March 2021, 2:01 pm

Kila ifikapo Machi 8 Dunia huadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Siku hii huadhimishwa kwa namna mbalimbali Ulimwenguni ikiwa na Lengo la kutambua mchango wa Mwanamke katika Nyanja mbalimbali.

Katika kuzingatia hili Sauti za Watangazaji wa kike tu ndio zitasikika Pangani FM katika vipindi vyote leo.

Meneja wa Pangani FM Bi. Maimuna Msangi

“katika kuendelea kumsherehekea mwanamke na leo tupo katika siku maalumu ya wanamke basi wanawake viongozi wa pangani fm redio ambao ni watangazaji na waandishi wa habari watahusika katika vipindi vyote ambavyo tupo navyo katika siku ya leo kwahyo mwanamke wa pangani fm siku ya leo atasimama katika vipindi vyote ambavyo hata vilikuwa vikifanywa na watangazaji wa kiume”,

Amesema Meneja wa Pangani FM Bi Maimuna Msangi

Na kwa upande wao baadhi ya watangazaji wa kituo hiki Mtumwa Kombora na Mwanaidi Jumanne wameelezea namna walivyojipanga kuiadhimisha siku hii kwa kufanya vipindi ambavyo vimezoeleka kufanywa na Wanaume ikiwemo kipindi cha Jahazi la Michezo.

“siku ya leo nimejipanga vizuri kwasababu nmeamsha kipindi cha Asubuhi ya leo lakini badae nitafanya kipindi cha michezo cha jahazi la michezo na tunaweza kufanya vizri kuliko hata wanavyofanya wanaume”

Amesema Mwanaidi Jumanne

katika siku hii ya leo niwaambie wanawake ni siku ya kubadilishana uzoefu kuweza kujadili changamoto zetu kuzizungumza na kutafuta njia mbadala zakuweza kukabiliana nazo,tutakuna saa mbili kamili usiku kwenye jahazi la michezo yani tutakiwasha”

Amesema Mtumwa Kombora