Pangani FM

Baraza la Wazee Tanga rasmi, Pangani ina wazee wachache zaidi.

4 February 2021, 7:55 pm

WATUMISHI wa ngazi zote mkoani Tanga wameaswa kuacha kudharau na kuwanyanyapaa wazee pindi wanapofuata huduma kwenye ofisi zao badala yake kuwanyenyekea na kuwapa kipaumbele ili kupata Baraka.

Hayo yamesemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martin Shigela wakati akizindua baraza la wazee la mkoa huo ambapo amewataka watumishi popote watakapokuwa kuwaheshimu na kuwanyenyekea wazee kwani ndiyo hazina pekee inayoleta Baraka ndani ya Taifa.

Sikiliza hapa taarifa ya Mwanahabari wetu Rajabu Mustapha

Kwa mujibu wa taarifa rasmi viongozi wa wazee Mkoa Mwenyekiti ni Hasheem Shekilindi,Makamu Mwenyekiti ni Felista Njogele, Katibu John Kiondo, Katibu Msaidizi ni Ismail Mrope.

Mikoa mitano inayoongoza kwa wazee wengi Tanzania ni 1.KILIMANJARO 2. MTWARA 3. LINDI 4. PWANI 5. TANGA ambapo wazee ni 6.9% ya idadi ya watu.

Kwa Mkoa wa Tanga Wilaya inayoongoza kwa kuwa na Wazee wengi ni Lushoto na Wilaya yenye wazee wachache zaidi ni Pangani.