Pangani FM

Halmashauri ya Wilaya ya Pangani yaanzisha ‘Benki ya Matofali’

2 February 2021, 8:38 pm

Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga imeanzisha kampeni maalum ya ‘Benki ya matofali’ kwa lengo kuwezesha kila kijiji kuandaa matofali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

Mkurugenzi wa Halashauri ya Wilaya Pangani Bw. Isaya Mbenje

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani BW ISAYA MBENJE katika mahojiano na Pangani FM.

 “Kila kijiji kikifanikiwa kutengeneza tofali 1000 kwa mwaka mmoja siku wakitaka kujenga jengo lolote lile kama zahanati wanachukua tu tofali na kama wanahela kidogo ya kumlipa fundi na kununua Saruji kazi inakuwa rahisi na watendaji wa vijiji tutawapima katika hili,viongozi wengine kama wenyeviti na madiwani tunaomba waunge mkono ili tukipata miradi kutoka serikalini tusipate shida”

Amesema Bwana Isaya Mbenje

Pia BW MBENJE amewataka Wananchi ,kamati za Shule na bodi za Shule kuendelea kusimamia miradi mbalimbali ya shule ili iweze kukamilika kwa wakati

“Tunaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ,tunaomba kamati za shule za msingi na sekondari tunaomba kamati za shule endeleeni kusimamia shule zenu miradi hii ikikamili kwa wakati itasaidia watotowetu kusoma vizuri”

Amesema Bwana Isaya Mbenje