Pangani FM

Uhusiano kati ya Chakula Shuleni na Utoro.

26 January 2021, 12:18 pm

Ukosefu wa chakula cha uhakika katika shule za msingi na Sekondari hapa Wilayani Pangani mkoani Tanga unatajwa kuchangia utoro kwa wanafunzi.

Hayo yamesemwa na Afisa Elimu Msingi Wilayani hapa ndugu JUMA HASSANI MBOHELA katika kikao cha kamati ya lishe ya Halmashauri ya Wilaya kilichowakutanisha wadau wa Elimu, Afya, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi na mipango.

Amesema kuwa baadhi ya wanafunzi wanaotoka maeneo yaliyopo mbali na shule wanakutana na changamoto hiyo hivyo ni wajibu kwa wadau kuangalia upya utaratibu wa   uchangiaji chakula Shuleni.

’unakuta Mtoto anakua mtoro shuleni ni kigurusimba akija shule anakaa siku nzima bila ya kula chakula chochote hadi usiku akirudi nyumbani, lazima aingie uvivu wa kuhudhuria shuleni, leo atakuja kesho ataacha kuja .

Amesema Afisa Elimu huyo.