Pangani FM

Kilimo cha Mkonge kwa Wakulima wadogo Pangani.

8 January 2021, 7:58 pm

Baadhi ya wakulima wadogo wilayani Pangani mkoani Tanga wameeleza kuhamasika katika a  kilimo cha Zao la Mkonge ili kujikwamua kiuchumi.

Wakizungumza katika kipindi cha Jicho Pevu kinachoruka kupitia Pangani FM kila siku ya Ijumaa kuanzia saa 12 Kamili Jioni kilichoangazia fursa ya kilimo cha zao la Mkonge, miongoni wakulima hao wamesema zao hilo linaweza kuwa mkombozi kwao kutokana na kuwa na uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo wapo walioonesha hali ya wasiwasi katika kujiingiza kilimo cha zao hilo wakihofia gharama kubwa ya uzalishaji wake.

Kwa upande wake afisa kilimo umwagiliaji na ushirika wilaya ya Pangani Bwana Ramadhani Zuberi amesema mkulima anaweza kumudu kilimo hicho kwa kuchanganya zao la Mkonge na mazao mengine ikiwemo mahindi.

Sikiliza hapa Makala hiyo ya Jicho Pevu.