Pambazuko FM Radio

Vyama vya ushirika Ifakara vyalia kucheleweshwa kwa mikopo, kutozwa riba kubwa

1 June 2023, 2:33 pm

Wajumbe wakiwa kwenye kongamano la vyama vya Ushirika{Picha na Elias Maganga

Na Elias Maganga

Viongozi wa vyama vya ushirika na SACCOS katika halmashauri ya mji wa Ifakara wamemweleza  mkuu wa wilaya ya Kilombero changamoto zanazowakabili ikiwa ni pamoja na wavuvi walioomba soko la Kivukoni, na kumiliki mabwawa ya asili bila mafanikio pamoja na mikopo inayotolewa na taasisi za fedha kutozingatia muda na kutozwa riba kubwa.

Mwenyekiti wa Kongamano la Vyama vya Ushirika Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bakari Mkangamo{Picha na Elias Maganga}

Changamoto hizo zimetolewa na  mwenyekiti wa kongamano la vyama vya ushirika Bakari Mkangamo  kwenye kongamano la vyama vya vya ushirika halmashauri ya mji wa Ifakara liliofanyika kwa lengo la Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstun Kyobya kujitambulisha kwa vyama hivyo,

Sauti ya Mwenyekiti wa kongamano la vyama vya ushirika Bakari Mkangamo 

Akiwasilisha risala kwa mgeni rasmi, Afisa Ushirika wa halmashauri ya mji wa Ifakara Bwana Issa Kilua ameelezea hali ya vyama vya ushirika katika halmashauri hiyo kuwa hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu, jumla  vyama vya ushirika 36, ambapo 12 kati ya hivyo ni vyama vya akiba na mikopo, vyama vya mazao na masoko 20, vyama vya ushirika vya uvuvi 3, chama kikuu kimoja na chama cha mradi wa pamoja kimoja, vyote hivyo  vikiwa na jumla ya wanachama 10,572.

Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bwana Issa Kilua{Picha na Elias Maganga]

Aidha Bwana Kilua amesema hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu serikali imewezesha vyama vya ushirika kuwadhamini katika taasisi mbalimbali za kifedha na kuweza kukopa zaidi ya bilioni 14.

Sauti ya Afisa Ushirika wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bwana Issa Kilua

Mkuu wa wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya  akijibu changamoto zilizowasilishwa  na vyama vya ushirika ,amesema wavuvi wajengewe mabwawa ya kisasa na atazungumza na TAWA kuhusu soko la kivukoni na watajibiwa ndani ya muda mfupi

Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya{Picha na Elias Maganga}
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya

Pia mkuu huyo wa wilaya akazungumzia changamoto ya mikopo kwa vyama vya ushirika

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya

Aidha ameziagiza  AMCOS zote  kuajiri wataalam kutokana na changamoto walizonazo ndani ya miezi mitatu toka sasa. Amemwagiza pia Afisa Ushirika kiundwe chombo kitakachosimamia vyama vya ushirika vyote ndani ya wilaya ya Kilombero huku akisisitiza mikutano ya vyama hivyo  vifanyike mara mbili kwa mwaka.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya

Kongamano hilo liliobeba kauli mbiu isemayo  “Ushirika ni Biashara, Ushirika kwa Maendeleo Endelevu” lilitanguliwa na maandamano yaliyopokelewa na mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Kilombero Wakili Dunstan Kyobya

Picha wajumbe wa kongamano wakiwa katika maandamano{Picha na Elias Maganga}
Sauti za nyimbo za maandamano,Mkuu wa Wilaya akipokea maandamano