Pambazuko FM Radio

mafuriko ya haribu miundombinu ya barabara na makazi ya watu Ifakara

27 April 2023, 11:44 pm

Mvua za masika zinazoendelea kunyesha Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro zimesababisha mafuriko na athari katika baadhi ya maeneo ikiwemo kitongoji cha Kwa shungu, kata ya Mbasa na Lumemo kata ya Lumemo halmashauri ya mji wa Ifakara.

Na; Isidory Mtunda

Namna mafuriko yalivyo athiri makazi – ( Picha na: Katalina Liombechi)

Kata sita za halmashauri ya mji wa Ifakara wilaya Kilombero mkoani Morogoro zimeathiriwa na mafuriko kutokana na  mvua zilizonyesha usiku wa  Jumamosi kuamkia  Jumapili Aprili 23, 2023.

Wakizungumza na Pambazuko fm Aprili 23, 2023 baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Kwa shungu, kata ya Mbasa halmashauri ya mji wa Ifakara, Imelda Malema, Hilda Chikopa na Jenifa Makayula wamesema mafuriko hayo yamesomba Unga, mchele Maharagwe na Magodoro pia yameribu mazao.

moja ya kaya zilizoathiriwa na mafuriko – Picha na: Katalina Liombechi

Waathirika hao wameomba uongozi wa halmashauri ya mji wa Ifakara, hususan kama ya maafa kupeleka msaada wa haraka wa chakula na mahitaji mengine muhimu katika kaya zilizokumbwa  na mafuriko hayo.

sauti za waathirika wa mafuriko

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kitongoji cha kwa shungu bwana Shabani Msowale amesema kuwa robo tatu ya kitongoji hicho  kimeathiriwa  na mafuriko hayo na ameoimba serikali ya wilaya hiyo kupeleka wataalam haraka kwa ajili ya kufanya tathmini ya athari   zilizotokana na mafuriko hayo.

Mwenyekiti wa kitongoji cha kwa shungu – picha na Katalina Liombechi
sauti ya mwenyekiti wa kitongoji

Kwa upande wake mratibu wa maafa halmashauri ya mji wa Ifakara Brigita Haule, amesema madhara yaliyosababishwa na mafuriko hayo ni pamoja na, uharibifu wa miundo mbinu ya barabara na makazi ya watu.

Bi Haule amesema mafuriko hayo yameathiri barabara ya Ifakara kidatu, nyumba nane zilizopo kata ya Lumemo , shule ya msingi Maendeleo na shule ya sekondari kwa Shungu zenyewe zimezingirwa na maji.

sauti ya mratibu wa maafa

Bi Haule ameishauri jamii kuchukua tahadhari za kiafya kwa kunywa maji yaliyochemshwa, kunawa mikono kwa sabuni na kula vyakula vya moto ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindu pindu. 

sauti ya mratibu
watoto kucheza kwenye maji ya mafuriko inaweza kuhatarisha afya zao – Picha na: Katalina Liombechi

Mratibu huyo ametaja maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo kuwa ni kata za; Mbasa, Viwanja sitini, Mwaya, Kidatu Lumemo na Kata ya Ifakara.