Pambazuko FM Radio

Bibi wa miaka 62 anusurika kifo bada ya kuangukiwa na nyumba

21 April 2023, 8:48 pm

Bi Hamida Kitage mwenye umri wa miaka 62 amesema ilikuwa majira ya saa tisa alasiri akiwa ndani ya nyumba hiyo ya tofali za kuchoma alisikia kitu kimedondoka kutoka juu na kumpiga kichwani na kudondoka

Na Elias Maganga

Mkazi wa mtaa wa viwanja sitini magengeni katika halmashauri ya mji wa Ifakara Wilayani Kilombero Bi Hamida Kitage amenusurika kifo baada ya nyumba anayoishi kumuangukia akiwa ndani,

Akisimulia tukio hilo Bi Hamida Kitage mwenye umri wa miaka 62 amesema ilikuwa majira ya saa tisa alasiri akiwa ndani ya nyumba hiyo ya tofali za kuchoma alisikia kitu kimedondoka kutoka juu na kumpiga kichwani na kudondoka

Amesema baada ya kudondoka alipiga kelele kuomba msaada ambapo majirani walimtoa katika nyumba hiyo  na kumpeleka zahanati ya Nico kwa matibabu ambapo hali yake inaendelea vizuri kwani alitibiwa na kuruhusiwa

Picha ya Bi Hamida Kitage {Picha na Elias Mganga}
Sauti ya Bi Hamida Kitage

Afisa mtendaji wa Mtaa wa Viwanja Sitini Magengeni Bi Sophia Msiku amethibisha kuanguka kwa nyumba hiyo na kuongeza kubwa Mama huyo anaishi na watoto wake na wakati tukio hilo linatokea watoto hawakuwepo walikuwa shamba,

Amesema nyumba hiyo imebomoka na kumwangukia mama huyo imetokana na mvua kubwa za Masika zinazoendelea kunyesha

 Picha ya Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Viwanja sitini Magengeni Bi Sophia Msiku{Picha na Elias Maganga}

               

Sauti ya Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Viwanja sitini Magengeni Bi Sophia Msiku