Pambazuko FM Radio

Wanaushirika wakubaliana kuongeza hisa pamoja na michango-Kilombero

5 April 2023, 3:53 pm

Wanachama wa Chama cha Ushirika cha Uvuvi,Usindikaji  na Masoko Kilombero wakiwa kenye mkutano

Chama cha Ushirika cha Uvuvi,Usindikaji  na Masoko Kilombero kimeundwa kwalengo la kuwaunganisha Wavuvi wote wanaojihusha na Uvuvi na hio itasaidia kudhibiti uvuvi haramu ili kuulinda Mto Kilombero unaopeleke maji kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere kwa asilimia 65

Na Elias Maganga

Chama cha Ushirika cha Uvuvi,Usindikaji  na Masoko Kilombero kimewataka wananchama wake kuongeza hisa kutoka moja ama mbili hadi kufikia kumi pamoja na kuongeza michango ya kila mwezi kutoka shilingi 3000 hadi 10,000

Akiwasilisha taarifa kwa wananchama katika mkutano uliofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Kitambaa Cheupe uliopo Iipangalala katika Halmashauri ya Mji  wa Ifakara,Mwenyekiti wa Ushirika huo Abubakary Mashamba,amesema sasa umefika wakati kwa ushirika huo kukimbia kuelekea maendeleo ya chama hicho,hivyo kuna kila sababu wananchama kuongeza hisa na michango hiyo.

Bwana Mashamba amewaeleza wanaushirika kuwa wasiponunua hisa wala kuchangia michango ya kila mwezi hawataweza kuundesha ushirika na badala yake utakufa.,pia ameeleza mikakati na mwelekeo wa ushirika katika kipindi cha mwezi April-June mwaka huu uanze kukopeshana kupitia hisa ,wadau na tasisi za kifedha na serikali kuu.

Mwenyekiti wa Ushirika Kilombero Bwana Abubakary Mashamba{Picha na Elias Maganga}

Sauti ya Mwenyekiti wa Ushirika Kilombero Abubakary Mashamba akitoa taarifa kwa wanaushirika

Hata hivyo amesema Taasisi za kifedha kama vile Benk ya NMB na  Equit Bank zipo tayari kufanyakazi na chama cha ushirika cha uvuvi,Usindikaji na Masoko Kilombero hivyo amewaomba wanachama waridhie ujio wa benki hizo na wadau wengine watakaopatikana

Sauti ya Mwenyekiti wa Ushirika Kilombero Abubakary Mashamba akielezea ujio wa tasisi hizo za kifedha

Wanachama waliohudhuria mkutano huo kwa pamoja wamekubaliana kuongeza hisa na michango ya kila mwezi ya shilingi elfu kumi huku wakitoa angalizo kwa wananchama wasiochangia kufuata katiba inavyoeleza.

                  Anolda Mkumba ni mwanaushirika waliosshiriki mkutano {Picha na Elias Maganga}

Mwanaushirika akiwaomba wajumbe watakaopatikana ifanye kazi kwa bidii

Mkutano huo pia umemteua Bwana Elias Maganga kuwa mkuu wa Kitengo cha Habari na mawasiliano, ambapo amewakumbusha wajumbe Katiba ya chama hicho inampa Mamlaka Mwanachama kumteua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya kulipwa hisa,akiba,amana na faida zote za chama na hapa anaelezea sifa za mwanachama

    Mkuu wa Kitengo cha Habari na mawasiliano  Elias Maganga akisisitiza wanachama kufuata katiba