Pambazuko FM Radio

Waadventista Wasabato Ifakara wachangia Damu

21 March 2023, 7:20 pm

Waumini wa kanisa la Wasabato wakichangia damu{Picha na Katalina Liombechi}

Kutokana na changamoto ya upatikanaji wa Damu katika maeneo ya kutolea huduma za Afya,Waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato-Ifakara wamejitokeza kuchangia Damu ili kuiunga mkono Serikali.

Na Katalina Liombechi

Jumla ya Chupa 36 za Damu zimepatikana baada ya watu waliojitokeza kuchangia Damu kwa Hiari zoezi lililoandaliwa na Waumini wa Kanisa la Waadventista wasabato katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara ikiwa ni Maadhimisho ya wiki ya matendo ya Huruma.

Zoezi hilo limefanyika katika eneo la Kanisa lililopo Maendeleo, wamechangia Damu na kwamba wapo tayari kujitoa kwa ajili ya watu wengine.

Mwenyekiti wa Conference ya Mashariki Kati Wa kanisa hilo Nchini Tanzania Mchungaji Deogratius Bambaganya amesema Wanaamini kuangalia na kuwasaidia wahitaji katika kujitoa kwa ajili ya kuokoa uhai.

Mwenyekiti wa Conference ya Mashariki Kati Wa kanisa hilo Nchini Tanzania Mchungaji Deogratius Bambaganya{Picha na Katalina Liombechi}
Sauti ya Mchungaji Deogratius Bambaganya akielezea uchangiaji wa Damu

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Adam John akizungumza kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Wakili Danstan Kyobya amewapongeza waumini wa Kanisa hilo kwa tukio kubwa la kuisaidia serikali kuchangia Damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa Damu kwa Haraka.

Aidha ameahidi kuendelea kuwapa ushirikiano Waumini hao kwa mambo mbalimbali wanayoyafanya huku akitumia Hadhara hiyo kutoa wito kwa Makanisa mengine na Jamiii kwa ujumla kufanya matendo ya huruma.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Adam John{Picha na Kataliana Liombechi}
Sauti ya Katibu Tawala Adam akiwapongeza waumini wa Kanisa hilo kwa tukio kubwa la kuisaidia serikali kuchangia Damu

Mteknolojia wa Maabara kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisko Ifakara Edda Mwandoloma amewashukuru waumini hao kwa kuchangia Damu chupa 36 huku akitoa wito kwa jamii kuchangia kwani bado uhitaji ni mkubwa kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya wajawazito na watoto,waliopata ajali,Sikoseli na Magonjwa Mengine.

Sauti ya Mteknolojia wa Maabara kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Fransisko Ifakara Edda Mwandoloma akitoa takwimu za waliochangia Damu

Wakizungumza baadhi ya Vijana waliochangia Damu akiwemo Neema Makambi,Brevin Osca,Eva Soni na Lucas Patrick Wamesema wameguswa kuchangia Kutokana na kuwa na moyo wa utayari wa kuwasaidia wengine kwani wamesema kanuni za ukristo ni pamoja na kuwasaidia watu wengine.

Brevin Osca ni mmoja kati ya wachangiaji damu{ Picha na Katalina Liombechi}
Vijana waliochangia Damu akiwemo Neema Makambi,Brevin Osca,Eva Soni na Lucas Patrick wakielezea namna walivyoguswa kuchangia Damu

Ikumbukwe kuwa Waumini wa Kanisa la Waadventista wasabato kila mwaka katika Wika ya pili kwenda ya Tatu ya mwezi March huadhimisha wiki ya matendo ya Huruma ambapo kwa mwaka huu wamefanya matendo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchangiaji wa Damu pamoja na kusaidia vitu mbalimbali kwa wagonjwa wa kituo cha Afya kibaoni.