Pambazuko FM Radio

Rais Dr Samia atoa milioni 65 ujenzi wa zahanati

23 February 2023, 3:09 pm

Na Elias Maganga

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzan imetoa fedha Milioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kata ya viwanja sitini katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara.

Akizungumza na Pambazuko FM, ilipotembelea mradi huo hii leo February 23 mwaka hu, Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo Bwana William Kawawa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi hicho cha fedha huku awamu ya kwanza wakipatiwa milioni 40.

Ujenzi huo unatarajiwa kukamilika baaada ya wiki mbili toka sasa.

Habari zingine kutoka pambazuko

Ujenzi wa  zahanati kukamilika hivi karibuni

Chanjo ya kichaa cha Mbwa

Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Viwanja Sitini Mjini Ifakara Bwana William Kawawa{Picha na Elias Maganga}

Bwana Kawawa amesema kukamilika kwa zahanati hiyo inategemea na fedha zinazotolewa na Serikali, ambapo kwa hatua ya boma ujenzi huo unatarajiwa kukamilika baaada ya wiki mbili toka sasa.

Sauti ya Mwenyekiti wa Ujenzi Bwana William Kawawa akielezea ujenzi huo

Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Viwanja sitini Maria Johnson Mkuvalwa amesema ujenzi huo ulianza tangu mwaka 2017 lakini ulisimama kutokana na changamoto ya upatikanaji wa fedha.

Afisa Mtendaji wa kata ya Viwanja sitini Maria Johnson Mkuvalwa {Picha na Elias Maganga}

Bi Maria amesema katika awamu hii ya kwanza Mbunge wa Jimbo la Kilombero Mheshimiwa Abubakari Asenga alitoa msaada wa mifuko hamsini ya saruji, tripu 15 za kifusi na fedha kiasi cha shilingi milioni tano na baadae Raisi Dr samia aliwapa milioni 65 huku awamu ya kwanza ya ujenzi huo wakipewa milioni 40.

Sauti ya Afisa Mtendaji wa kata ya Viwanja sitini Maria Johnson Mkuvalwa akielezea changamoto na mwenendo wa ujenzi wa zahanati ya viwanja sitini

Kwa upande wake Katibu wa Mbunge Jimbo la Kilombero Bwana Saidi Libenanga amesema tangu kuanza kwa ujenzi huo ulisuasua kutokana na viongozi waliokuwepo wakati huo  kuchangisha fedha na kugawana kama posho na hivyo wananchi kususia ujenzi huo.

Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kilombero Said Libenanga{Picha na Elias Maganga}

Sauti ya Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Kilombero Said Libenanga akielezea namna ujenzi huo ulivyosuasua hapo awali