Pambazuko FM Radio

Wanufaika wa Tasaf walia kuondolewa kwa ruzuku-Ifakara

18 February 2023, 1:18 pm

Na Elias Maganga

Wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya Jamii Tasaf awamu ya tatu Kata ya Mbasa katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara wamekuwa na hali ya sintofahamu juu ya ruzuku ya msingi na utekelezaji wa mradi wa barabara huku  baadhi ya wanufaika wakisitishiwa malipo.

Baadhi ya wanufaika wa TASAF wa kata ya Mbasa {Picha na Elias Maganga}

Wakizungumza na Pambazukofm baadhi ya wanufaika wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf awamu ya tatu,wamesema awali walielezwa kuwa miradi ya jamii inayotekelezwa na wanufaika hao,ambapo kimsingi malipo yake ni shilingi elfu tatu kwa siku wanashangazwa kuondolewa kwa ruzuku ya shilingi 24000 ambayo huwa wanalipwa baada ya miezi miwili.

Sauti za wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini wa Kata ya Mbasa Halmashauri ya Mji wa Ifakara wakilalamikia kuondolewa kwa
sehemu ya ruzuku

Akitolea ufafanuzi Mratibu wa mfuko wa maendeleo ya jamii Tasaf kwa ngazi ya Halmashauri ya mji wa ifakara Bi Brigita Haule amesema kuwa kwasasa wako katika awamu ya tatu ya utekelezaji wa mpango wa kunusuru kaya masikini  katika awamu hii tasafu imejikita sana kutoa ruzuku kwa wananchi wenye hali duni kimaisha na kwa kata ya Mbasa wanatekeleza mradi wa Barabara

Habari zingine kutoka Pambazuko FM

Mikakati ya kuondokana na uchafu wa mazingira yaanza kutekelezwa-Ifakara

Zoezi la uondoaji Mifugo limeanza katika Bonde la Mto Kilombero

Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bi Brigita Haule{Picha na Elias Maganga}
Sauti ya mratibu wa TASAF Halmashauri ya Mji wa Ifakara Bi Birgita Haule akitoa ufafanuzi wa Tasaf awamu ya Tatu

Kuhusu kuondolewa kwa ruzuku kwa baadhi ya wanufaika wa Tasaf,Bi Brigita amesema kaya yoyote inayotakiwa kufanya kazi katika mradi wa barabara  kuna sehemu ya ruzuku inasitishwa

Sauti ya mratibu wa TASAF Brigita Haule akilelezea kuhusu kuondolewa kwa ruzuku kwa baadhi ya wanufaika

Baadhi ya wanufaika kuondolewa kwenye mpango huo wa kunusuru kaya masikini Bi Brigita amekanusha na kusema hakuna mtu aliyeondolewa kwenye mpango huo isipokuwa kuna baadhi ya wanufaika wamesitishiwa malipo na hiyo inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya mlengwa kutofika kwenye kituo cha kupokelea  malipo,kifo na wale wanaostahili kufanya kazi za miradi ya kijamii.

Sauti ya Brigita Haule mratibu wa TASAF akifafanua kuhusu Baadhi ya wanufaika kuondolewa kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini

Ikumbukwe kuwa Kipindi cha Pili awamu ya tatu wa mpango wa kunusuru kaya masikini kitafikia malengo yake kwa kutekeleza shughuli mbali mbali kupitia sehemu kuu tatu ambazo ni uhawilishaji fedha ambao utaongeza kipato cha kaya na kuwekeza katika afya na elimu ya watoto, kuinua uchumi wa kaya kwa kujenga uwezo kwa kaya katika utunzaji rasilimali na kutengeneza njia mbadala na endelevu za ajira na kushiriki katika kazi za jamii na kupata kipato cha ziada kwa matumizi ya kaya kama chakula na kugharamia mahitaji mengine ya msingi na wakati huo wakiboresha miundombinu katika jamii na kupata ujuzi na stadi za maisha.