Pambazuko FM Radio

Wazazi wamekubaliana kuchangia lishe shuleni

10 February 2023, 3:07 pm

Wazazi wakiwa kwenye kikao{picha na Katalina Liombechi}

Na Katalina Liombechi

Wazazi wa watoto wanaosoma katika Shule ya msingi Ifakara katika Kata ya Viwanjasitini Halmashauri ya Mji wa Ifakara wamekubaliana kuchangia lishe kwa watoto pindi wanapokuwa Shuleni ikiwa ni njia ya kukuza Ufaulu Shuleni hapo.

Katika Makubaliano hayo wazazi wamesema watachangia kila mzazi shilingi 1600 kwa Mtoto mmoja kutokana na kutambua umuhimu wa kufanya hivyo.

Sauti za wazazi wakijadili kuchangia lishe katika shule ya msingi Ifakara

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Esther Nuruva amesema watoto wanapokosa kupata lishe pindi wanapokuwa shuleni inapelekea kutokuwa na usikivu mzuri kwa mwalimu

Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ifakara Esther Nuruva{Picha na Katalina Liombechi}
Sauti ya Mwalimu mkuu Esther Nuruva akizungumza na wazazi

Kwa Upande wake Mratibu Elimu kata ya Viwanjasitini Edwin Mkonga amesema kila mzazi anawajibu wa kuhakikisha mototo wake anapata lishe pamoja na huduma zingine muhimu kwani serikali inawajibika kwa Elimu Bure na mambo mengine.

Mratibu Elimu Kata Mwalimu Edwine Mkonga {Picha na Katalina Liombechi}
Sauti ya Mratibu Elim Kata akizungumza na wazazi

Hata hivyo Mtendaji wa Mitaa ya Uwanja wa Taifa A,B,Viwandani Mhola na Viwanjasitini B,Ally Hassan Ally na Mwenyekiti wa Mtaa wa Uwanja wa Taifa A Charles Lyungu wamesema ni vyema wazizi wakatekeleza kwa hiyari waliyokubaliana kabla ya utekelezwaji wa Faini ya Shilingi elfu Hamsini.

Mwenyekiti wa mtaa wa uwanja wa Taifa A Bwana Charles Lyungu{picha na Katalina Liombechi}
Sauti ya Afisa Mtendaji Mtaa na Mwenyekiti wa Mtaa Ally Ally na Charles Lyungu wakizungumza na wazazi