Pambazuko FM Radio

Kambi Kusaidia Wanafunzi Wasichana Kutimiza Ndoto zao

25 June 2021, 6:14 am

Na; Katalina Liombechi

Mkurugenzi msaidizi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Susana Nyarubamba amesema ili msichana aweze kuwa salama jamii na wazazi wanatakiwa kutengeneza utamaduni wa kuwa walinzi wa watoto wao kila wakati wawapo shuleni ama nyumbani au mazingira yoyote ili aweze kuwa salama kuepukana na vishawishi na hasa matendo ambayo yanapelekea kuenea kwa maambukizi ya ukimwi.

Amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kambi ya wasichana rika balehe 220 kutoka shule za Sekondari 22 za kata wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Aidha Nyarubamba amesema Rais Wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kujenga shule za sekondari 1,000 kwa awamu nchi nzima kati ya hizo shule 26 maalumu kwa ajili ya wasichana, shule 717 za kata na nyingine za wenye mahitaji maalumu au ya kipekee na hiyo ni kabla ya kufika mwaka 2025 zitakuwa zimekamilika.

Mkurugenzi msaidizi wa Elimu ya Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Susana Nyarubamba

Akizungumza kwa aniaba ya wanafunzi wenzake Nuru salum amesema kambi hiyo itawasaidia sana kuepuka vishawishi mbalimbali na pia wanajifunza stadi za maisha na namna ya kujikinga kupata maambukizi ya virus vya ukimwi 

Mwanafunzi Nuru Salum