Orkonerei FM

Siku ya wanawake Arusha

10 March 2022, 9:22 am

Polisi wanawake Mkoa wa Arusha washerehekea siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada Mahabusu ya Watoto.

NA NYANGUSI OLE SANG’IDA

Afisa mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishina msaidizi wa Polisi (ACP) MARY KIPESHA ambae pia ni Mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake Mkoa wa Arusha (TPF NET) amewaongoza askari wakike Mkoa wa Arusha kutembelea mahabusu ya watoto na kutoa misaada mbalimbali katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Akiongea na watoto hao wakati akikabidhi misaada hiyo amesema wamefikia  uamuzi wa kutembelea mahabusu hiyo ya watoto kwa lengo la kuwaona, kuwafariji pamoja na kusikiliza changamoto zao wakiwa kama wazazi na wasimamizi wa sheria.

Awali mtandao huo wa polisi wanawake waliungana na wanawake wengine Mkoa wa Arusha kusherehekea kilele hicho cha siku ya wanawake duniani kwa kufanya maandamano yaliyoanzia katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha hadi katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo mgeni rasmi alikua Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongela