Orkonerei FM

Bilioni 1.5 mradi wa maji Terrat Simanjiro

10 March 2022, 7:14 pm

wananchi wa kijiji cha terrat wakiwa katika mkutano wa kutambulishiwa mradi wa maji katika kijiji chao.
kaimu meneja wa RUWASA wilaya ya simanjiro mkoa wa manyara akizungumza na wananchi wa kijiji cha terrat wilaya ya simanjiro katika kutambulishiwa mradi wa maji.
Diwani wa kata ya terrat mh.jackson materi akizungumza na wananchi wa kijiji cha terrat wakati wakitambulishiwa mradi wa maji katika kijiji chao.
mwenyekiti wa kijiji cha terrat .bw.kone penet medukenya akizngumza na wananchi wa kijiji cha terrat katika mkutano wa kutambulishiwa mradi wa maji.

HABARI. na pascal sulle

Kaimu meneja wa Ruwasa wilaya ya simanjiro Eng.  Johanes Martine  amesema serikali imetoa kiasi cha fedha bilioni 1.5 kwa ajili ya kuleta mradi wa maji  katika kata ya terat yenye vijiji vitatu na vijiji hivyo vyote vitapata mradi huo.

Akizungumza katika mkutano wa kijiji cha terrat Eng. Johanes Martine amesema tokea siku ya jumanne tumekuwa tukitambulisha mradi huu mkubwa wa maji katika vijiji vitatu ambavyo ni engonongway,nadonjukin na kijiji cha terrat ambapo kwa kila kijiji kina kisima inayozalisha maji mengi na kazi kubwa ni kujenga matenki makubwa katika kila kijiji ili watu waweze kupata huduma hii ya maji.

Amesema mradi huo utatekelezwa kwa miezi sita kuanzia mwezi huu wa tatu na utamalizka kabla ya mwezi wa kumi na tayari mkandarasi atakaefanya hiyo kazi ameshasaini mkataba na kuanzia tarehe 17 na 18 mwezi wa tatu atakabidhiwa majukumu yote kwa ajili ya kuleta vifaa na kuanza kazi.

Kwa upande wake diwani wa kata ya terrat Jackson Materi ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya raisi samia suluh hasan kwa kutoa fedha ya utekelezaji wa mradi huu mkubwa wa maji ndani ya kata ya terrat ambapo kwa mda mrefu vijiji hivyo visima vyake vingi havikuwa vinafanyakazi kutokana na kutokuwa na miundo mbinu ya umeme lakini kwa hivi sasa visima vyote vitafufuliwa kutokana na bajeti kubwa ambayo serikali imeileta katika kata ya terrat.

Mwenyekiti wa kijiji cha terrat bw. Kone Penet Medukenya  amesema tumeupokea mradi huu wa maji katika kijiji cha terrat na serikali ya kijiji umeupokea pamoja na wanachi wote kuupokea na kutokana na serikali kusema haitafidia maeneo au miundombinu ambayo yatatumika katika kuupitisha mradi huo wa maji bado koramu kubwa ya wananchi wamekubali miundo mbinu hiyo kupitishwa katika maeneo yao.