Nuru FM

Kitomo akabidhi Printer shule ya Msingi Nyamihuu

15 May 2023, 1:16 pm

Elia Kitomo wa kwanza kutoka upande wa kulia akikabidhi Printer katika shule ya Msingi Nyamihuu Mkoani Iringa.

Na Hafidh Ally

Mdau wa maendeleo Elia Kitomo amekabidhi mashine ya kuprint na kutoa copy katika shule ya msingi Nyamihuu ili iwasaidie katika shughuli za Kitaaluma.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hiyo, Elias Kitomo ambaye ni Mkurugenzi wa Kitomo Hardware inayojihusisha na usambazaji wa Vifaa vya ujenzi, amesema kuwa ameamua kurejesha kwa Jamii hasa katika shule hiyo ili Walimu waweze kufanya kazi ufanisi.

Amesema kuwa mashine hiyo ina thamani ya shillingi milioni moja na itasaidia walimu kuandaa mitihani, ya wanafunzi wa shule ya Nyamihuu na shughuli za kiofisi shuleni hapo.

Hata hivyo amewasihi wadau wengine kuendelea kuisaidia shule ya Nyamihuu ili iweze kukua Kitaaluma.

MWISHO