Nuru FM

Mashindano ya mbio za magari kufanyika msitu wa Sao Hill Iringa Mei 13

11 May 2023, 10:50 am

Waratibu wa mbio za magari mkoani Iringa wakizungumza na wanahabari kuhusu mashindano hayo. Picha na Fabiola Bosco

Na Fabiola Bosco

Mashindano ya mbio za magari yanayofahamika kwa jina la CMC Automobile Sao Hill Forest Rally of Iringa yanatarajiwa kuanza tarehe 13 mwezi wa tano katika Misitu ya asili Sao Hill .

Kwa mujibu wa mwandaaji mkuu wa mashindano hayo Robert Maneno amesema wamedhamiria kufanya mashindano ya mbio za magari tarehe 14 mwezi Mei yanayohusisha washiriki kutoka Tanzania na nje ya Tanzania toka Kenya ,Uganda na Zambia.

” Tarehe kumi na tatu kutakuwa na maonesho pale uwanja wa Samora kisha tarehe 14 itakuwa ni kilele hapa katika shamba la Sao Hill na mashindano yamekamilika tunashukuru pia kwa muhifadhi kwa kufanya maandalizi mpaka saa hizi Kuna gari 12 na washiriki kadhaa mwingine kutoka Tanzania wengine kutoka nchi za jirani Kama Zambia,Kenya na mwingine kutoka Uganda na wameanza safari Yao kuja hapa Iringa na Kuna gari ambao nafikiri tunategemea italeta vionjo japo zote zitaleta vionjo Ila gari itakayokuwa Kali ni Fordfiesta R5 ambao itatumiwa na mtu kutoka Uganda “

Moja ya washiriki wa Mbio za magari katika shamba la Sao hill

Amjad Khan ni mwenyekiti wa mashindano ya mbio za magari zitakazofanyika Misitu ya Saohill alisema kuwa pamoja na mashindano hyao kufanyika wanatarajia kupokea ugeni mkubwa huku aliwataka washiriki kutumia vizuri sheria watakazopatiwa n mamlaka ya Misitu .

“Mpaka Sasa tumefikia asilimia 90 safari hii tunategemea kupata ugeni mkubwa Sana wanakujaniwa sababu sio mashindano tuu Bali wankauja kuangalia pia mashindano katika shamba kwa hiyo hiyo siku itatujengea jina kubwa tunashukuru kwa watu wa Saohill kwa kutupokea mashabiki wa gari karibuni Sana haya ni tofauti na Yale tuliyokuwa tukifanya zamani kikubwa tuzingatie sheria tutakazopewa ikiwemo sigara hapa marufuku mazingira tuache yakiwa safi “.

Naye PCO Tebby Yoramu Kaimu muhifadhi mkuu wa shamba la miti Saohill alisema kuwa mashindano hayo yatakuwa fursa ya kuonyesha utalii uliopo ndani ya shamba la miti Saohill ikiwa ni pamoja na utalii wa nyuki , uvuvi na maporomoko yaliyopo ndani ya Hifadhi ya shamba Hilo.

“Tunashukuru na kufirahi kwa kuona Saohill inafaa kwa mashindano ya mbio za.magari hii ni fursa za vivutio kwa ajili ya utalii wa tiolojia kwa sababu ukitaka kuangalia hapa tunavyanzo vya utalii vingi ikiwamo tunamizinga ya nyuki ,Manzuki , na hapa Kuna uoto wa miti ya kupandwa ,wanyama pia mimea ,pia itakuwa chanzo Cha utalii kwa sababu Kuna maporomoko ya maji ,bwawa la ngwazi,uvuvi wa kurejesha pia utalii wa makasia na mashindano haya huenda yakafungua pia fursa ya mashindano mengine Kama mashindano ya baiskeli, marathon”.

Shamba la miti Saohill sio tuu kwa ajili ya mashindano ya mbio za magari pia utalii wa uoto wa asili na usio wa asili ,utalii wa bwawa la ngwazi ,Uvuvi wa kurejesha ,utalii wa makasia na mto Ruaha huku ikiwa na fursa kwa wawekezaji wengine.