Nuru FM

Polisi Iringa wamshikilia Tegete kwa Kulawiti Mtoto.

8 May 2023, 2:11 pm

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Issa Suleiman akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Mwandishi wetu

Na Joyce Buganda na Hafidh Ally

Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa linamshikilia Kijana anayejulikana kwa jina la DRIVE TEGETE Mkazi wa kijiji cha kidamali kata ya mzihi mwenye umiri wa miaka 23 kwa kosa la kulawiti Mtoto.

Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP ISSA SULEIMAN amesema mtuhumiwa huyo alimrubuni Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 8 wakati akicheza mpira na wenzake.

Sauti ya Kaimu Kamanda Issa

“Mtuhumiwa huyo alimchukua mtoto huyo na kisha kumpeleka kwenye shamba la mahindi na kisha kutenda tukio hilo na kumuacha huko na kuondoka” Alisema Kamanda Issa

Katika tukio lingine Kmanda Issa amebainisha kuwa Jeshi la polisi katika kipindi cha mwezi Aprili limepata mafanikio ya kesi tofauti ikiwemo kuwashikilia watu watano na tayari wameshukumiwa mahakamani akiwemo kijana aliyejulikana kwa jina la Ayoub Msigwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita.“

pia kuna mshtakiwa Baraka Mwinuka amehukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka, mshtakiwa Wilbert Mpyagisa amehukumiwa jela miaka mitano kwa kosa la kuua bila kukusudia” alisema Kamanda Issa

Hata hivyo Jeshi la polisi Mkoa wa iringa linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano pindi wanapoona matuikio ya kihalifu katika jamii.