Nuru FM

Miradi ya Bilioni 4.9 yakubaliwa na Viongozi wa Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Mufindi

2 May 2023, 7:47 pm

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dkt.Linda Salekwa akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo na Viongozi wa mbio za Mwenge kitaifa. Picha na Mwandishi wetu.

Na Mwandishi wetu.

Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 umeridhia miradi yote katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa miradi yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 4.9.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo yote Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Abdalah Shaibu Kaim amesema ameridhishwa na utekelezaji wa miradi yote ambayo imepitiwa na mwenge huo.

Aidha Abdalah amewataka watumishi wote kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo ili miradi ikamilike kwa wakati na wananchi waanze kunufaika na miradi hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe.Dkt.Linda Salekwa amesema maagizo na maelezo yote yaliyotolewa na kiongozi huyo kama Wilaya ameyapokea na atahakikidha yanafanyiwa kazi kwa manufaa ya wananchi wa Mufindi na Taifa ujumla.

Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 ni Mradi wa Mazingira Shule ya Wasichana ya Mufindi,Kuweka jiwe la Msingi Shule ya Sekondari Mbalamaziwa,Nyololo ugawaji wa Ng’ombe na maziwa,Nzivi klabu ya kupambana na rushwa,Kasanga kuweka jiwe la Msingi jengo la upasuaji na Mkalala jiwe la Msingi Mradi wa Maji .