Nuru FM

Shule ya Sekondari Mtwivila yapewa Computer na Runinga na Kampuni ya Vodacom.

26 April 2023, 11:16 am

Viongozi wa Kampuni ya simu ya Vodacom wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego. Picha na Joyce Buganda

Na Joyce Buganda

Kampuni ya simu za mkononi VODACOM TANZANIA kwa kushirikiana na mradi wa AFRICAN CHILD PROJECT wametoa komputa 6,router na luninga 1 katika shule ya Sekondari Mtwivila Manispaa ya Iringa huku wakisisitiza walimu kutumia zaidi teknolojia ili kuwa fanya wanafunzi kuwa kidigitali.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo shuleni hapo mkuu wa kampuni ya VODACOM nyanda za juu kusini BI HAPINESS SHUMA amesema lengo lao kuu ni kuwasaidia walimu na wanafunzi kujifunza na kupata vitabu kwa njia ya kimtandao.

Sauti ya Happiness Mkuu wa Vodacom

PASCHAL MUSA ni mwakilishi na msimamizi wa mradi wa AFRICAN CHILD PROJECT amesema kwa mkoa wa iringa ni shule 14 ndo zimefikiwa na mradi huo.

Sauti ya Pascal kutoka African CHILD Protection

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya sekondari mtwivila DAINES MYALA ameishukuru kampuni ya VODACOM TANZANIA kwa kuwapatia msaada huo kwani kutawafanya wanafunzi waelwele zaidi.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa iringa HALIMA DENDEGO amewapongeza wadau hao na kusema wao kama serikali wataendelea kushirikiana nao ili kuendelea kuiweka dunia kiganjani.