Nuru FM

Iringa yaanza kutekeleza afua za lishe kutokomeza udumavu kwa watoto

26 April 2023, 11:48 am

Picha ya mfano wa mtoto akipata Lishe Bora.

Na Adelphina Kutika

Mkoa wa Iringa wenye asilimia 59.9 ya udumavu umeanza kutekeleza mpango wa utekelezaji wa afua za lishe zinazolenga kukabiliana na changamoto hiyo na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano.

Afisa lishe mkoa wa Iringa Anna Nombo amesema katika kupunguza udumavu kwa watoto wameendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa lishe kutekeleza afua zinazoleta matokeo makubwa katika siku 1000 za kwanza za maisha ya mtoto.

Sauti ya Afisa Lishe

IBRAHIMU SINDANI ni baba wa watoto watatu amesema baada ya kupata kipeperushi cha lishe katika mtaa wake kinachomhamasisha kushiriki maadhimisho ya afya na lishe amechukua jukumu la kushiriki ili kujifunza namna ya kuandaa lishe kwa watoto wake.

Sauti ya baba akizungumzia kuhusu Lishe

Kwa upande wake Afisa Elimu Kata ya Gangilonga mwalimu wiliam kyando amesema kuwa kutokana na utekelezaji wa mkataba wa lishe wamefanikiwa kwa asilimia 75 ya kuhakikisha watoto wa kata yake wanapata chakula shuleni.

Hata hivyo serikali nchini Tanzania inatarajia kutenga shilingi bilioni 67.2 kwajili ya kutekeleza mpango jumuishi wa lishe ya taifa wa pili wa miaka mitano2021 /2022 hadi 2025/2026.