Nuru FM

Kete 58 za dawa za Kulevya aina ya Heroine zakamatwa Iringa

3 April 2023, 3:05 pm

Madawa ya Kulevya aina ya Heroin yamekatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Iringa baada ya Mtuhumiwa kuumwa Tumbo.

Na Fabiola Bosco/ Joyce Buganda

Jeshi la polisi mkoani wa Iringa linamshikilia Mwasema Rashid (37) mkazi wa Tabata Magengeni Jijini Dar es Salam akiwa na kete 58 za madawa ya kulevya tumboni mwake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa kijana huyo amekamatwa baada ya kuumwa tumbo na hivyo kwenda zahanati ambapo alibainika kuwa na madawa hayo aina ya Heroin.

Alisema kuwa Mwasema Rashid aligundulika kuwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin aliyokuwa akisafirisha kuelekea nchini Msumbiji baada ya kuitumia usafiri wa anga.

Kamanda Bukumbi amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na hali mbaya na kumsaidia kutoa kete hizo kwa njia ya haja kubwa chini ya uangalizi wa madaktari na Jeshi la polisi.

Kupitia taarifa hiyo kijana Macdonald Zuberonga (23) mkazi wa Semtema na Hatuna mbigili (24 ) mkazi wa wa ipogolo walikutwa na madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni bhangi kete (324) na majani makavu aina ya bhangi ambayo yalikutwa sehemu wanazoishi .

Katika hatua nyingine Kamanda huyo amebainisha kuwa wamekuta silaha aina ya shortgun yenye namba za usajili TZCAR 88980 ikiwa imetelekezwa katika vichaka vya msitu wa Saohil wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa.