Nuru FM

Deni la serikali lazidi kupaa lafikia Trilion 71.31

29 March 2023, 7:55 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Hesabu za serikali. Picha kwa msaada wa Mtandao

Deni la Serikali kufikia June 30,2022 lilikuwa Tsh. Trilioni 71.31 ikilinganishwa na Tsh. Trilioni 64.52

Na Mwandishi wetu

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali – CAG, Charles Kichere amesema hadi kufikia Juni 30, 2022 deni la Serikali lilikuwa ni Shilingi 71.31 Trilioni.

CAG Kichere ameyasema hayo hii leo Machi 29, 2023, wakati wa akiwasilisha ripoti ya ofisi yake kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam.

“Deni la Serikali kufikia June 30,2022 lilikuwa Tsh. Trilioni 71.31 ikilinganishwa na Tsh. Trilioni 64.52 lililoripotiwa kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kuna ongezeko la Trilioni 6.79 sawa na 10.5%, ambapo kipimo cha deni la Serikali kinachotumia pato la Taifa kinaonesha Deni hili ni himilivu” alisema

Akiongelea deni hilo, Rais Samia asema, “mwenendo wa Deni la Serikali tunakopa ndio, tunakopa kwa maendeleo lakini tunakopa kwa akili, tusipokopa hatutofanya maendeleo lakini lazima tukope mikopo yenye unafuu tufanye maendeleo.”