Nuru FM

Watoto 172 Iringa Wanufaika Bima ya Afya

27 March 2023, 12:52 pm

Mkurugenzi wa Makutano Tv akitoa neno la shukurani.Picha na Adelphina Kutika.

Watoto 172 mkoani Iringa wamekabidhiwa bima za afya ili kuweza kumudu matibabu pindi wanapokabiliwa na magonjwa.

Na Adelphina Kutika.

Taasisi  isiyo ya kiserikali ya Rounding Hands to Save Community na Makutano TV kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Iringa na Hidaya Catering mkoani Iringa wamekabidhi kadi za bima 172 kwa watoto wenye Mahitaji maalumu.

Akisoma taarifa ya Utekelezaji wa zoezi hilo Mkurugenzi wa Taasisi ya Rounding Hands to save Community Bi Jesca Mwalyoyo katika tukio la mtoto Bima lililofanyika katika viwanja vya kituo Cha Nyumba Ali  ameeleza lengo la kutoa bima hizo ni kuwawezesha watoto kupata matibabu kwa wakati.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Rounding Hands to save Community Bi Jesca Mwalyoyo akitoa taarifa ya utekelezaji.

Akijibu taarifa hiyo Balozi wa watu wenye Ulemavu Tanzania na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Iringa DK Ritha Kabati   ameahidi kulipia bima za afya  kwa watoto zipatazo 150 zilizosalia.

Balozi wa watu wenye Ulemavu Tanzania na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Iringa DK. Ritha Kabati akitoa ahadi.

 ‘’Tujitahidi kutoa misaada  mbalimbali kwa kushirikiana na wafadhili na watu wengine  wenye mapenzi mema, lakini uhitaji  ni mkubwa,hivyo tunawaomba  watanzania na wadau wengine wajitokeze kuwasaidia watoto wenye ulemavu,’’alisema Ritha.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa watu wenye ulemavu Shaaban Shomary na Zawadi Msigala wameiomba serikali kuhakikisha wanawasaidia upatikaji wa fursa nyingine Ili kutimiza malengo Yao na sio bima pekee .

Mwenyekiti wa watu wenye ulemavu Shaaban Shomary na Zawadi Msigala akitoa ombi kwa serikali.

Akitoa Shukurani kwa wadau waliofanikisha zoezi hilo Mkurugenzi wa Makutano Tv Tukuswiga Mwaisumbe amesema kipindi cha corona hali ya watoto ilikuwa hairidhishi ndio sababu iliyopelekea kuwawezesha bima hizo.

Mkurugenzi wa Makutano Tv Tukuswiga Mwaisumbe akitoa neno la shukurani.

Hata hivyo wanufaika wa bima hizo ni   watoto  kutoka Shule ya Msingi Ipogolo kitengo maalum na Shule ya Msingi saba saba kitengo maalum ambapo tukio hilo limetanguliwa na  maonyesho ya utoaji wa huduma ya elimu kwa watoto wenye ulemavu.

Uhitaji  ni mkubwa,hivyo tunawaomba  watanzania na wadau wengine wajitokeze kuwasaidia watoto wenye ulemavu.