Nuru FM

Wasanii Wakemea Ukatili Iringa

13 March 2023, 12:21 pm

Mwenyekiti  Mweza wa Tasisi  ya Shada Organization Shamsa Ford akizungumza katika mkutano huo.Picha na Adelphina Kutika.

Kufuatia matukio ya kikatili yanayoendelea kushamiri katika mkoa wa Iringa wasanii wenye asili ya Iringa wameamua kuungana kutengeneza filamu yenye maudhui ya kupinga ukatili.

Na Adelphina Kutika.

Wasanii maarufu  wa filamu nchini ambao  asili yao kutoka  mkoa wa Iringa  wamesema wapo katika hatua za mwisho  za kuandaa filamu ambayo maudhui yake yatakuwa kupinga ukatili wa kijinsia uliokithiri mkoani hapa.

Akizungumza na kituo hiki  Mwenyekiti  wa taasisi ya shada organization inayojishughulisha na masuala ya kupinga ukatili wa kijijnsia nchini Halima Yahya Mpinge  maarufu kama (DAVINA) amesema kuwa  wamekwisha kuanza maandalizi  ya awali ya kuandaa filamu hiyo ili kutoa elimu kwa umma kama sehemu ya kuunga mkoani juhudi za serikali awamu ya sita kwenye mapambano dhidi  ukatili wa kijinsia .

Mwenyekiti  wa taasisi ya Shada Organization Halima Yahya Mpinge  maarufu kama (DAVINA) akielezea mikakati waliyoandaa.

“watoto wanaangamia sasa hivi,watoto wadogo  wanafanyiwa vitendo vya kikatili,watoto wakiume wanaharibiwa wakiwa wadogo  ,kwahiyo wazazi tuungane  kukemea haya matendo taifa linaangamia”alisema

Shamsa Ford ni Mwenyekiti  Mweza wa Tasisi  ya Shada Organization amesema kuwa kutokana na tatizo la ubakaji na Ulawiti kuwa kubwa  wameamua kushirikiana na wasanii wa mkoa wa Iringa kuhakikisha wanaanda filamu itakayotoaelimu ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mwenyekiti  Mweza wa Tasisi  ya Shada Organization Shamsa Ford akieleza mpamgo wa kuwashirikisha wasanii Iringa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Filamu mkoa wa Iringa Hamis Nurdin  amesema kuwa lengo la kutengeneza filamu hiyo ni kwajili ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia  na ulawiti.

Mwenyekiti wa Filamu mkoa wa Iringa Hamis Nurdin akieleza lengo la kuandaa filamu hiyo.

wazazi tuungane  kukemea haya matendo taifa linaangamia.