Nuru FM

Polisi Watoa Elimu Kukemea Ukatili Iringa

7 March 2023, 4:27 pm

Mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia Elizabeth Swai akiwaasa wanafunzi wa shule ya msingi Azimio.Picha na Joyce Buganda.

Kufatia kukithiri kwa matendo ya kikatili katika mkoa wa Iringa Jeshi la Polisi linaendeleza kampeni ya kutoa elimu ya kutokomeza ukatili.

Na Joyce Buganda.

Jeshi la polisi Mkoani Iringa linandelea na kampeni ya kutoa elimu katika makundi mbalimbali  kuhusu mambo ya ukatili yanayoendelea mkoani hapa.

Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa ASP Allan Bukumbi alipokuwa katika shule ya msingi Azimio manispaa ya Iringa amewaasa wazazi na walezi kuongeza usimamizi kwa watoto na kuwajenga kimaadili ikiwa ni pamoja na kuwatimizia mahitaji yao ya msingi.

kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa ASP Allan Bukumbi akiwaasa wazazi kuwa na malezi bora.

Mossi Ndosero ni mkuu wa kitengo cha usalama barabani mkoa wa Iringa amewaasa watoto kutembea kwa umakini wawapo barabarani pamoja na kuacha kucheza barabarani kwani watoto wengi kuanzia miaka mitano wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani huku wengine wakipata ulemavu wakudumu.

 Mkuu wa kitengo cha usalama barabani mkoa wa Iringa Mossi Ndosero akiwaasa watoto kuwa makini barabarani.

Kwaupande wake mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia Elizabeth Swai amewaasa watoto kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili kama ubakaji,ulawiti, mimba za utotoni na ajira za utotoni.

Mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia Elizabeth Swai akiwaasa watoto kujilinda na matukio ya kikatili.