

3 March 2023, 4:18 pm
Wameomba elimu hiyo mara baada ya kupata usumbufu ambao wamekuwa wakipitia wakati mgumu wakifuatilia dhamana.
Na Joyce Buganda.
Wakazi wa Manispaa ya Iringa wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu kuhusu suala la dhamana ili kuwapunguzia adha pindi wanapohitaji huduma hiyo.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wananchi wamesema baadhi yao hawatambui vyema mchakato wa kupata dhamana kwa mtuhumiwa jambo linalosababisha usumbufu kwao hivyo kutolewa kwa elimu kutawasaidia kuokoa gharama.
Kuhusu suala hilo wakili Cleofas Mwailuka amsema mtu mwenye kuanzia miaka 18 ana haki ya kumdhamini mtuhumiwa pia kuna elimu ya dhamana ambayo huwa inatolewa kila mwezi februali kila mwaka katika wiki ya sheria pamoja na kufanya majukumu mengine kuelimisha uma.
Aidha amtaja makosa kama ya mauaji uharifu kwa kutumia silaha na kutaka kuipundua serikali hayana dhamana na kuionya jamii kutojihusisha na makosa ya aina yoyote.
Kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 148 kifungu kidogo cha 5 kimeainisha makosa mengine ambayo mtuhumiwa akipewa dhamana ni hatari kwa usalama wake makosa hayo ni pamoja na ulawiti, utakatishaji fedha, kusafirisha dawa za kulevya na ugaidi.