Nuru FM

Wodi yazinduliwa Kilolo -Wanawake kunufaika

1 March 2023, 2:24 pm

Mwonekano wa chumba kimojawapo katika wodi iliyojengwa Ipalamwa.Picha na Joyce Buganda.

Wodi yenye thamani zaidi ya milioni 190 yajengwa Ipalamwa baada ya kuteseka muda mrefu kwa wananchi hao.

Na Joyce Buganda.

Zahanati ya Ipalamwa chini ya shirika la GLOBAL VOLUNTEER wilaya ya Kilolo imezindua wodi ya kinamama wanaotarajia kujifungua yenye thamani ya shilingi million 194 lenye uwezo wa kuwatunza kinamama 10 kwa wakati mmoja.

Akizungumza wakati wa kuzindua jengo hilo Mkurugenzi wa GLOBAL VOLUNTEER Nayman Chavala amesema jengo hilo limefadhiliwa na familia ya Peter J king kutoka  nchini marekani ambapo kina mama hao watajitunza na kuwatunza watoto wao.

Mkurugenzi wa GLOBAL VOLUNTEER Nayman Chavala akielezea kuhusu jengo hilo.

Aidha Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Ipalamwa Dokta  Sylas Mosha amesema kinamama  hao watapata   mafunzo ya lishe na kuwasaidia kinamama kuwa wazazi.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Ipalamwa Dokta  Sylas Mosha akishukuru kwa kujengewa wodi.

Kwa upande wao wanufaika  wa huduma  hiyo kutoka vijiji vya Makongo, Lulindi, Ukwega,Mkalanga na Ipalamwa  wamesema wanashukuru kwa kuwajengea wodi hiyo kwani vutapunguza  kasiya vifo vya mama na mtoto.

Wanufaika wakielezea furaha ya kujengewa wodi hiyo.