Nuru FM

 CCM Yawataka Wafanyakazi Kutimiza Wajibu 

22 February 2023, 2:04 pm

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa Daud Yassin akiongea na wajumbe wa mkutano huo.Picha na Adeliphina Kutika.

Serikali ya Mkoa wa Iringa imetoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Na Adeliphina Kutika.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa kimewataka wafanyakazi wa serikali kutambua wajibu wao wawapo kazini kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ili kuleta maendeleo yanayokusudiwa kwa wananchi.

Akizungumza wakati serikali ya mkoa wa Iringa ikitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha mapinduzi  (CCM)2020 kwa kipindi Cha mwezi julai 2022 hadi disemaba 2022,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa kutokea mkoanwa Iringa (MNEC) Salim Abri Asas amewataka wafanyakazi wa serika kutambua wajibu wao ili kuongeza ufanisi wao wa kazi kwaajili ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Asas alisema kuwa chama cha mapinduzi ndio kinabeba lawama  ya utekelezaji wa maendeleo “ubovu wa barabara anaetekeleza ni Tanroad lakin ukienda kwa wananchi wanasema ccm ndio hawajatekeleza ,sisi tunabebe lawama za watumishi katika utekelezaji wa maendeleo.

“watendaji wa serikali hakikisheni mnachapa kazi na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi kwani mkiulizwa na wananchi mnachofanya watumishi mnatoa nafasi kwa chama kutoa majibu ya maswali ya wananchi wanayohoji sisi ndio tunabeba lawama zenu kama kuna mahali pana shida tuambizane mapema”alisema Asas.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa (MNEC) Salim Abri Asas akiongea na wajumbe wa mkutano huo.Picha na Adeliphina Kutika.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa Daud Yassin alisema chama hicho kimeridhia taarifa hiyo ya utekelezaji kwa halmashahuri zote za mkoa wa Iringa huku akiwataka watendaji wote kutimiza wajibu wao katika kazi walizo pewa.

Yassin alisema kuwa kamati ya siasa mkoa ilitoa maagizo kwenye baadhi ya maeneo ambayo hayakufanya vizuri kuhakikisha wanarekebisha walipokosea katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi wa Chama Cha mapinduzi  (CCM)2020 kwa kipindi Cha mwezi julai 2022 hadi disemaba 2022, mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego alisema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 zaidi ya watumishi 230 wa kada ya Afya   mkoani Iringa wameajiliwa ajira mpya zilizotolewa na @ortamisemi hali iliyosaidia kuongeza ufanisi katika utendaji kazi  katika mkoa.

Dendego alisema kuwa sekta ya afya imefanikwa kuajiri watumishi wapya 236 ambapo Hospital ya Rufaa watumishi 39, kilolo dc 57,Iringa dc 58 ,Mufindi 35,Iringa Mc 28  na  Mafinga 29.

Aidha Dendego alisema kuwa  jumla ya shilingi bilioni 1.818 zimewezesha upatikanaji wa vifaa tiba mbalimbali ikiwemo mashine za kufulia nguo mashine na mashine za kuchuja damu.

“Watendaji wa serikali hakikisheni mnachapa kazi na kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi”

Alimazia kwa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayowapigania watanzania kwa kuleta maendeleo katika kila sekta hapa nchini.

Rukia Mkindu ni katibu wa CCM mkoa wa Iringa  alisema Halmashauri hiyo imegawa  Ilani kwa wakuu wa idara na vitengo pamoja na watendaji wa kata ili kuwawezesha  kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwani kwa mujibu wa katiba ilani ya Chama Cha mapinduzi  (CCM)ndio inayoongoza serikali .

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Costantino Kihwele alitoa wito kwa watendaji na madiwani  wa halmashauri zote kuhakikisha wanawasomea ilani ya Chama Cha mapinduzi  (CCM) wananchi  ili watambue maendeleo yanayofanywa kupitia Ilani.