Nuru FM

Mbunge aibana serikali kuhusu miundombinu ya usafiri kwa watu wenye ulemavu

7 February 2023, 11:25 am

Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt Ritta Kabati akiuliza Swali Bungeni Jijini Dodoma. Picha na Halfan Akida

Serikali ina Mpango gani wa kuweka Sheria kwa Wamiliki Wa Vyombo Vya Usafiri ili Kuwa Na Miundombinu Rafiki Kwa Watu Wenye Ulemavu.

Na Hafidh Ally

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi imewataka  Mamalaka ya Usafirishaji Ardhini LATRA na Mamlaka ya Viwango Tanzania TBS kuhakikisha wanawake miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu katika vyombo vya usafiri.

Hayo yamezungumzwa Leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Iringa Dkt. Ritta Kabati aliyetaka kujua Ni Lini Serikali Itaweka Sheria Ya Wamiliki Wa Vyombo Vya Usafiri Kuwa Na Miundombinu Rafiki Kwa Watu Wenye Ulemavu?

Naibu waziri wa Ujenzi Mh. Mwakibete akitoa ufafanuzi kuhusu Miundombinu kwa wenye ulemavu

Katika swali lake la Msingi Mh. Kabati alitaka kujua mpango huo utaanza kutekelezwa lini kwa sababu amekuwa balozi kwa kuwasemea watu wenye ulemavu ili wawekewe miundombinu Rafiki.

“Nampongeza Ritta kwa kuwa balozi wa watu wenye ulemavu, kwa kweli amekuwa akiwasemea watu hao, lakini natoa wito kwa wahusika kuweka miundombinu bora ili kundi hilo liweze kunufaika na rasilimali za nchi” Alisema Naibu waziri Mwakibete

“Nampongeza Ritta kwa kuwa balozi wa watu wenye ulemavu, kwa kweli amekuwa akiwasemea watu hao, lakini natoa wito kwa wahusika kuweka miundombinu bora ili kundi hilo liweze kunufaika na rasilimali za nchi” Alisema Naibu waziri Mwakibete

Mbunge Ritta Kabati akiuliza swali katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Akizungumzia kuhusu Hoja ya Mbunge Kabati aliyeuliza kuhusu mpango wa serikali kuwachukulia hatua wale ambao wanawanyanyapaa watu wenye ulemavu, Mh. Mwakibete amesema kuwa serikali itachukua sheria kali kwa wanaowanyanyasa watu hao.

Aidha Naibu waziri huyo amesema kuwa tayari Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga sheria  ya kuanzishwa kwa mamalaka ya usafiri na udhibiti ili kuweka miundombinu rafikikwa wajili watu wenye ulemavu.