Nuru FM

Vijana na wanawake washindwa kurejesha mikopo ya halmashauri

3 February 2023, 2:47 pm

Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwada Mwenye Kipaza sauti akizungumza jambo

Wanawake na Vijana wanatakiwa wapate elimu ya umuhimu wa kufanya marejesho ya mikopo inayotolewa na Halmashauri ili wafanye marejesho kwa wakati.

Na Ansigary Kimendo

Kutokuwepo kwa elimu ya umuhimu wa kufanya marejesho ya mikopo inayotolewa na Halmashauri imetajwa kuwa chanzo cha vijana na wanawake wajasiriamali kufanya vibaya katika marejesho.

Akizungumza na kituo hiki Diwani wa Kata ya Mkimbizi Mh. Eliud Mvela amesema kuwa viongozi hawapaswi kutumia nguvu  katika urejeshwaji badala yake itumike hekima pamoja na Elimu ili wajue umuhimu wake.

Sauti ya Mvela kuhusu Mikopo

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Lumuli Yohanes Mlusi amesema kuwa wanawake wamekuwa wakifanya vizuri katika kurejesha  mkopo, changamoto ipo kwa vijana ambao wamekuwa ni watu wa kuhama katika makazi yao.

Sauti ya Yohanes Mlusi

Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada amesema kuwa Zaidi ya shilingi milion 800 zimetolewa kwa vikundi mbalimbali vilivyopo manispaa ya iringa vikiwemo vikundi vya vijana, akina mama, na watu wenye ulemavu ili kuwainua kiuchumi.

“katika msimu huu halmashauri imetoa zaidi shilingi milioni 350 lakini pia kabla ya sasa tulitoa karibu milioni 480 hivyo katika kipindi hiki tumetoa zaidi ya shilingi milioni 800 kwenye vikundi vyetu vya halmashauri na vinaendelea kufanya uzalishaji”.Alisema Ngwada

“Katika kipindi hiki tumetoa zaidi ya shilingi milioni 800 kwenye vikundi vyetu vya halmashauri na vinaendelea kufanya uzalishaji”.

 NGWADA amesema kuwa  halmashauri imeendelea kutoa  mikopo kwa vikundi mbalimbali vinavyokidhi vigezo vya kupata fedha hizo.