Nuru FM

Timu ya Igowole FC yaibuka Mabingwa wa michuano ya Kihenzile Cup 2022

12 December 2022, 6:25 am

Timu ya Igowole FC imefanikiwa kuwa mabingwa wa mashindano ya Kihenzile cup and awards mwaka 2022 baada ya kuifunga Timu ya Nyololo Kwa Mikwaju ya Penalti baada ya kutoka sare ya kufungana goli 2-2 katika dakika 90 za mchezo.

Kwa ushindi huo Timu Hiyo ya Igowole imefanikiwa kujinyakulia kiasi Cha shilingi laki 5, Jezi seti 2, mipira miwili, Na T-shirt ambayo atavaa nahodha wa timu Hiyo.

Timu ya Nyololo iliyoambulia nafasi ya Pili imepewa kiasi Cha shillingi Laki 3, Jezi seti 2 na Mipira miwili pamoja na t-shirt Moja Kwa ajili ya Nahodha.

Mbunge wa Jimbo la Mufindi kusini Mh. David Kihenzile akizungumza na wananchi waliojitokeza katika Fainali ya Michuano ya Kihenzile Cup and Award- Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala na Utawala Bora Mh. Deogratius Ndejembi

Kwa mujibu wa Mdhamini wa Michuano Hiyo, Mbunge wa Jimbo la Mufindi kusini Mh. David Kihenzile, Mshindi wa Tatu ambaye Ni timu ya Mtwango baada ya kuifurusha timu ya Malangali Goli 7-0 amejunyakulia Shillingi Laki 1, Jezi seti 1 na T-shirt ya Nahodha.

Aidha Mh. Kihenzile amesema kuwa Lengo la michuano Hiyo ni kuibua vipaji vya vijana katika Jimbo lake na kuwaepusha na makundi hatarishi.

Mabingwa wa Michuano ya Kihenzile Cup and award Timu ya Igowole fc katika Picha ya pamoja na viongozi mbalimbali

Amesema kuwa atawasemea wanamichezo bungeni Ili serikali iweze kupunguza Kodi ya vifaa vya michezo Kwa Lengo la kuwatengeneza vijana Kwa faida ya Timu za Vijana.

Mh. Kihenzile alisema kuwa katika Kutambua mchango wa shule za msingi zilizofanya vizuri katika mitihani ya darasa la saba mwaka huu, ametoa zawadi kwa shule ya tatu za halmashauri ya wilaya ya Mufindi ili kuhamasisha Taaluma.

 

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika Fainali ya mchezo huo Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala na Utawala Bora Mh. Deogratius Ndejembi amempongeza Mh. Kihenzile Kwa kuanzisha mashindano Hayo huku akimtaka kuandaa Combine ya wachezaji waliofanya vizuri katika mashindano Hayo Ili waweze kuunda Timu ambayo itaenda kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Combine ya Chamwino Jijini Dodoma.

Mashindano Hayo yamehusisha Timu 16 kutoka katika kata za Jimbo la Mufindi kusini yameshuhudiwa na Mwandishi Nguli wa Habari za Michezo hapa Nchini Shaffih Dauda ambaye ameahidi kuwachukua vijana waliofanya vizuri Ili kuwapeleka katika vilabu vikubwa na kufanya majaribio.

Mamia ya mashabiki waliojitokeza katika uwanja wa shule ya Msingi Igowole kushuhudia Fainali ya Michuano ya Kihenzile Cup and award 2022

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu Tanzania bara NEC, Mh. Richard Kasesela amewapongeza washindi waliopatikana katika michuano hiyo ya Kihenzile Cup huku akiwasisitiza vijana watakaopata nafasi ya kuchaguliwa na Mwanahabari Dauda kwenda kufanya majaribio, kuonesha nidhamu na kufanya vizuri ili kuwashawishi Maskauti wengine kuja Mkoani iringa kutafuta wachezaji wenye vipaji vya Mpira