Nuru FM

Mlinzi wa chuo cha RUCCU Iringa aiba gari kwenye maegesho ya chuo

8 December 2022, 5:53 am

JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia David Richard mwenye umri wa miaka 23 kwa kuiba gari aina ya raum rangi ya Grey yenye namba za usajili T 702 DFV mali ya Gasper Abraham mwenye umri wa miaka 34
aliloiba katika eneo lake la kazi

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Iringa kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa wamemkamata kijana huyo baada ya taarifa za kuibiwa kwa gari hilo kutolewa na hivyo kupelekea jeshi la polisi kufanya doria ya kutosha na kuikuta wilaya ya kilolo mkoani hapa

“Tunamshikilia David Richard mwenye umri wa miaka 23 mlinzi wa RUCU aliiba gari hiyo ikiwa kwenye maegesho
lakini mmiliki alitoa taarifa kwenye jeshi la polisi na ndipo utaratibu wa kumtafuta ukaanza ndipo ilipokutwa kwa mtuhumiwa akiitumia wilaya ya kilolo “

Pamoja na hayo Allan Bukumbi alisema  kuwa  miongoni wa waharifu waliofanikiwa kuwakamata katika  msako walioufanya  walifanikiwa kumkamata ndugu Boni Kipalile kwa kosa la kukutwa na silaha aina ya shortgun yenye namba 14949 na risasi tatu moja ikiwa chemba huku wakimshikilia benadetha kipago umri wa miaka 61 akiwa na meno ya tembo na kiboko

“Ndugu waandishi wa habari kutokana na taarifa za siri kijiji cha kiponzero wilaya ya mkoa wa Iringa tulifanikiwa
kumkamata boni kipalile mkulima mkazi wa igangidungu anayetuhumiwa kujihisuisha na matukio mbalimbali ya kihalifu akizwa na silaha moja aina ya shortgun namba za usajili 14949na risasi tatu moja ikiwa chemba pamoja na hilo tunamshikilia benedetha kipago kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo na meno mawili ya kiboko

Aidha kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Iringa amewataka wananchi kujitokeza na kutambua mali zilizokamatwa kwa watuhumiwa Emmanuel Mnyeke (28) na Alfred Mkanula (25) ambao walikamatwa na mali za wizi ikiwa ni pamoja na pikipiki 6 aina ya sanlg ,boxer na honda

Katika kushighulikia changamoto mbalimbali jeshi la polisi mkoani iringa lilifanikiwa kumkamata Sebastian
Mahuwili (42) aliyehukumiwa kwa kesi ya kubaka mtoto wa miaka 6 na hivyo
kupelekea Kufungwa miaka 30 jela kutokana na ushahidi kukamilika.