Nuru FM

Jeshi la Polisi Iringa lakamata Mtambo wenye thamani ya Mil 250 Mali ya Wizi

13 October 2022, 4:31 pm

JESHI la Polisi mkoa wa iringa  limefanya operesheni na kukamata  mtambo (wheel loader cartepille ) katika kijiji cha Igingilanyi kata ya isimani  Wenye thamani ya  Shilingi Million mia mbili hamsini .

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa ACP Allan Bukumbi  amesema kuwa mtambo huo wenye  namba T 322 CAF ni mali ya kampuni ya DB SHAPRIYA & COLTD.

Aidha ameongeza kuwa mtuhumiwa  mmoja   wa tukio hilo amekamatwa ambaye  ni mwanaume mwenye umri wa miaka( 42) fundi  na mkazi wa Nduli akiwa na mali za wizi zilizofunguliwa kutoka kwenye mtambo huo.

Hata hivyo  mali alizokutwa nazo ni Engine model no 3126,Rejeta 01,Madguard 04,Hydrolic pipe,Wiring system pamoja na Fan Guard na Propeller shaft.

Katika tukio jingine ,jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata  Pius Miki Mkazi  wa wiloles kwa tuhuma  ya kunja  na kuiba katika nyumba ya ndugu yake Felix Miki ambapo baada ya mahojiano mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo na kuonyeshamali alizoiba katika nyumba hiyo.

Aidha vitu hvyo ni pamoja na Runinga aina ya Telefunken inchi 55,Jiko la umeme,Jokofu,Godoro,Sofa pamoja na mitungi ya gesi ya kampuni tofauti  ambapo watuhumiwa watafikiwa mahakamani  upelelezi utakapokamilika.

 

MWISHO