Nuru FM

Ahukumiwa maisha Jela kwa Kumlawiti Mtoto wa miaka 6 Iringa

26 September 2022, 1:41 pm

MAHAKAMA ya wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha mtu mmoja Ayubu Kiyanza mwenye umri wa miaka 22 mkazi wa eneo la Don Bosco Manispaa ya Iringa kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 6 aliyekuwa akisoma darasa la pili.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo tarehe 11/01/2021 na alimvizia mtoto huyo akiwa anatoa shuleni ndipo akamvuta kichakani huku akiwa ameziba mdomoili asipige kelele.

Baada ya Kufika Nyumbani Babayeke alimuona Mwanae akiwa mchafu tofauti na Alivyomzoea akitoka Shuleni na Ndipo akamuhoji na Mtoto akamueleza Baba yake kilichotokea.

Baada ya Kumsikiliza Mwanae baba alimwambia Mwanae ampeleke eneo alilofanyiwa ukitili na wakiwa Njiani walimuona Mtuhumiwa Ayubu Kiyanza na Ndipo Taratibu za kumkamata Zikafanyika.

Kesi hiyo number 10 ya Mwaka 2021 ilikuwa na Mashahidi watano akiwemo Daktari aliyethibitisha kuwa mtoto huyo alikuwa amelawitiwa.

Akisoma Hukumu Hiyo Hakim Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa Rehema Mayagilo amesema Mtuhumiwa amekutwa na hatia kutokana na Ushahidi uliotolewa Mahakamani Hapo.

Awali Mwendesha Mashtaka wa Serikali Veneranda Masai aliiomba mahakama kutoa Adhabu Kali kutokana na kitendo kilichofanyika kimemuathiri Mtoto huyo.

Aidha Mahakama ilimpa nafasi ya Kujitetea Mtuhumiwa aliiomba mahakama kumpunguzia Adhabu kwa sababu anamtoto Mdogo na anamtegemea.

Hata hivyo mahakama Ikamuhumu kifungo Cha Maisha kwa kosa la kumlawiti mtoto Mdogo mwenye Umri wa Miaka 6 ambaye alikuwa Akisoma Darasa la Pili.

MWISHO