Nuru FM

EWURA Yatangaza Kushuka Kwa Bei Ya Mafuta Hapa Nchini

7 September 2022, 7:12 am

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini ambapo bei hizo zimeanza kutumika kuanzia leo Septemba 7, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi Modestus Lumato imesema bidhaa za mafuta ya mafuta katika soko la dunia za Julai 2022 zimepungua ikilinganishwa na bei hizo kwa Juni 2022.

Amesema kuwa  bei za mafuta katika soko la ndani zimepungua vilevile kwa kati ya shilingi 271/lita na shilingi 362/lita kwa petroli na kwa shilingi 430/lita kwa mafuta ya taa ukilinganisha na bei zenye ruzuku za Agosti 2022. Kwa mafuta ya dizeli, ukiiacha bei ya

Kwa kutoa ruzuku hiyo, Serikali imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa mwezi Septemba 2022 kwa Dar es Salaam bei i za Mafuta kwa mwezi Septemba 2022 kabla na baada ya ruzuku Petroli shilingi 3049 baada ya ruzuku shilinh 2969 na Dizeli shilingi /lita 3359 baada ya ruzuku shilingi 3125.

Mhandisi Lumato amesema kuwa Mafuta katika soko la dunia zimepungua ikilinganishwa na bei za mwezi Juni 2022 na kufanya kwa bei za mafuta katika soko la ndani zimepungua kati ya shilingi 271 kwa lita na shilingi 362 kwa lita kufikia kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia na ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani.

Amesema kuwa Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa Septemba 2022 ambapo bei hizo zinatofautiana kutokana na umbali kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kadri ya umbali unapokuwa mrefu ruzuku yake inakuwa kubwa.

Bei za mafuta kabla ya ruzuku, Agosti 2022 baada ya ruzuku pamoja na Kiwango cha Ruzuku kwa Petroli kwa mkoa wa Dar es Salaam bei petroli 3636 baada ya ruzuku 3410 kiwango cha ruzuku 220 hivyo mfano huo kwa Mkoa huo inaonyesha sehemu nyingine beo zinapanda kutokana na umbali.

Kwa taarifa hiyo ilibainisha kuwa katika kutekeleza bei hizo wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta watatakiwa kuzingatia kwa EWURA kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za

Amesema kuwa Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko na EWURA hiyo itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

Taarifa hiyo ilisema bei zinazotolewa lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta na Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za EWURA za kupanga bei za Mafuta za mwaka 2022 zilizotangazwa.