Nuru FM

BREAKING NEWS:Ilala Yapata Pigo Diwani Wake Afariki Akiwa Katika Ibada Msikitini.

8 July 2022, 7:29 am

CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimepata pigo kufuatia Diwani wake wa Kata ya Mahohe Mohamed Ngonde, kufariki leo alfajili

Akizungumza kwa njia ya simu Katibu wa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Busoro Pazi, alisema Marehemu Mohamed Ngonde alifariki akiwa katika Ibada ya alfajili Leo Julai 08/2022 akiwa msikitini.

Katibu wa Madiwani Busoro Pazi alisema taratibu za mazishi bado kila wakati atakuwa anatoa taarifa baada kukaa na familia ya marehemu.

“Kwa Sasa tunafanya taratibu za kwenda kuifadhi mwili wa marehemu katika hospitali ya Rufaa Mkoa Amana “alisema Busoro.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde alisema taarifa za Kifo cha MH, Diwani wake Mohamed Ngonde aliyefariki alfajili katika alizipata kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM kata Majohe ambapo alisema alimweleza kuwa Marehemu Mohamed Ngonde alifariki ghafla.

Mwenezi CCM Wilaya ya Ilala Alhaj Said Sidde alisema kila wakati atakuwa anatoa taarifa kamili kuhusiana na msiba huo mzito kwa Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na wana CCM kwa ujumla.

 Alhaj Said Sidde,pia ongeza kuwa alimwelezea Mh Ngonde kuwa kada mahiri aliyekitumikia Chama Cha Mapinduzi kwa muda mrefu na kushikilia nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti serikali ya mtaa Kichangani ,Majohe